October 22, 2012

KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA LWIKA KATIKA VIKUNDI VYA WAKULIMA

Bonde la mto Lwika lipo katika kijiji cha Lundo na linatengenisha vijji viwili, Lundo na Ngindo. Bonde la mto Lwika linafaa sana kwa kilimo cha Mpunga na Miwa. Katika kuboresha maisha ya wananchi kilimo cha miwa kimekuwa na nafasi kubwa kama ilivyo kwa kilimo cha Mpunga. kwa sasa wakulima wanaweza kutumia zana za kisasa ikiwemo Matreka. Pichani Trekta la Kikundi cha Umwagiliaji cha LWIKA. Treka hilo limenunuliwa kupitia Mpngo wa Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo katika Wilaya ya Nyasa(DADPS). Kilimo ni uti wa mgongo kwa wakazi wengi wa Wilaya ya Nyasa ikiwemo Mahindi, Mtama, Ulezi, uvuvi na mengineyo. Kikundi cha wakulima wa eneo hilo kimepewa ekari 2200. 

Picha ya Hoops Kamanga idara ya maendeleo Wilaya ya Nyasa.

Huyu ni mzee Mputa, ambaye alikuwa afisa Uvuvi, kwa sasa ameshastaafu. Hapo alikuwa katika ukaguzi wa kilimo cha Mpunga katika bonde la mto Lwika.


3 comments:

  1. HAKUNA SIKU NILIYOFURAHI KAMA LEO..KWANZA KUSIKIA LWIKA,NGINDO NA BILA KUSAHAU LUNDO KWANGU..NA KIKUBWA ZAIDI KUMWONA MZEE MPUTA..NI BABA YAKE MKUBWA RAFIKI YANGU KLARE MPUTA...

    ReplyDelete
  2. ha ha ha ha! Jambo zuri sana kukumbushana na kupeana taarifa. Kwa hakika nyasa inasonga mbele. ingawa ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini sasa tunasonga mbele

    ReplyDelete
  3. hahaha! hata mm pia nimefurahi kwa kumuona mjomba angu Mzee mputa mwana samaki akiwa katika bonde la mto lwika ambako enzi hizo nilikuwa tunafungia mbuzi na ngo'mbe, na kuroposha mango'ndo na manga'cho.

    ReplyDelete

Maoni yako