October 22, 2012

UJENZI WA ZAHANATI KATIKA WILAYA YA NYASA

Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mbaha baada ya kukamilika kwa ukaratabati wake. Kijiji chicho kipo katika Kata ya Mbaha, kwenye Tarafa ya Ruhuhu iliyopo wilaya mpya ya Nyasa. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo, kama inavyosemwa MTU NI AFYA.

Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Luhindo likiwa katika awamu ya kwanza ya kukamilisha kuwa kituo kidogo cha afya. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo katika wilaya ya Nyasa

Jengo linalofuata hapo chini  ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mitawa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Kijiji chicho kipo katika  wilaya mpya ya Nyasa. Hii ni harakati ya kusogeza huduma  za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo kwa wananchi, ingawa juhudi zinahitajika. 
 Ujenzi wa Zahanati ya ya Kijiji cha Mkali kilichopo katika Kata ya Lipingo, kwenye Tarafa ya Ruhekei iliyopo wilaya mpya ya Nyasa.  Ujenzi wa kituo hicho unaendelea.


Katika jamii yoyote suala la kupiga hatua ni muhimu sana. Na jamii haiwezi kupiga hatua kama haijaanza kutengeneza hatua husika. ili mafanikio yapatikane ni lazima juhudi zifanyike, ni muhimu kutunza kile kinachoanza kutengenezwa ili tuweze kuboresha. Pengine Zahanati hizi zisiwe na kiwango bora cha huduma za afya. lakini ni heri kuanza kwa hatua hiyo kuliko kutokuwepo kabisa. Nchi yako kwnaza.
PCIHA ZOTE NA Hoops Kamanga, Nyasa

2 comments:

  1. Nimekumbuka kweli Lipingo, mkali..we acha tu...nimefurahi pia kuona maendeleo yake ya Wilaya hii mpya..

    ReplyDelete
  2. Bila shaka, kwa juhudi kubwa zinazoendelea hakuna shaka mambo yatakuwa mazuri zaidi ifikapo Juni mwakani au desemba mwakani. hali imebadilika sana na kuna fursa mpya za kilimo, biashara, uchumi, uvuvi na kahdalika. nyasa inabadilika sana tena kwa kasi. nadhani kuanzisha wilaya mpya ni kusogeza huduma kwa wananchi

    ReplyDelete

Maoni yako