November 28, 2012

LIULI YAHIFADHI HISTORIA YA JIWE LA POMONDA

Jiwe la Pomonda
Miongoni mwa miji muhimu katika wilaya ya Nyasa ni mji wa Liuli. Mji huu unayo bandari muhimu ambayo hutumiwa na meli zinazofanya safari katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. meli za Mv Iringa na Mv Songea zimekuwa zikitia nanga katika bandari hiyo ikiwa ni sehemu ya kukuza uchumi, usafirishaji bidhaa na kadhalika. 
Katika rekodi za kihistoria kuna mengi ya kukumbukwa katika mji wa Liuli, lakini jambo muhimu ni kuwepo kwa Jiwe hilo ambalo linalinganishwa na sura ya binadamu. Ukkchunguza jiwe hilo utaona linafanana kidogo au kuwa na maumbile fulani yenye sura ya binadamu. 
Ni historia nzuri na tamu kwa wakazi wa nyasa na vitongoji vyake. Jiwe hilo lipo karibu kabisa na Bandari ya Liuli ambapo kila abiria au msafiri yeyote anapotumia bandari hiyo ataweza kuliona. Ni moja ya vivutio vya Utalii katika mji wa Liuli. KARIBUNI WATALII, KARIBUNI LIULI kujionea mengineyo.

2 comments:

  1. Hi, for all time i used to check web site posts here early in the break of day, because i love
    to learn more and more.
    Also visit my website ; how to download movies

    ReplyDelete
  2. kaka kwa kweli blog imependenza sana.pia waweza tembelea yangu.www.mosesnsuha.blogspot.com alafu unipe marekebisho ambayo utayagundua katika blog yangu! kazi njema.

    ReplyDelete

Maoni yako