Na Markus Mpangala, Dar es Salaam
Kuna dhana moja kwamba vyama vya upinzani ni uadui. Kimsingi
jambo hilo sio kweli na lazima tukemee kuwa kazi ya vyama vya upinzani ni
kuikumbusha serikali kupitia chama kinachotawala. Hivyo basi kazi ya serikali
ya CCM ni kuhakikisha kuwa masuala ya msingi ndani ya nchi yanafanyika
ipasavyo.
Haiwezekani wapinzani wakaibuka tu kutoka porini na kuanza kupinga
ama kulalamikia jambo fulani. Lazima wameketi chini na kuona namna ambavyo CCM
inakosea na makosa hayo ni dosari tu ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi. Vivyo hivyo
kazi ya CCM sio kulalamika kuwa kwanini wapinzani hawashiriki kutatua kero ya
nchi yetu. Kazi ya vyama vya upinzani ile kukosoa na kukishambulia CCM maana
yake wanatimiza wajibu wa kuikumbusha serikali ya CCM kuwa kuna mahali hapaendi
vizuri.
Kwahiyo Kazi ya mpinzani ni kukupinga. Dosari yako ni faida kwake. Yapo
maeneo ambayo vyama vyote vinapaswa kushirikiana, mathalani lile kongomano lililoandaliwa
na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuhusu ulinzi, usalama na demokrasia,
mbali ya Chadema kususia. Lakini neno kubwa hapa ni kwamba mpinzani akiona
dosari zako ndio kete yake ya kupata ushindi.
Ukitaka mpinzani wako asipate
kete ya ushindi hakika unaziba mianya yote ya kumfanya apate kete. kwanza,
hakika Ilani ya chama chako inatekelezwa, ahadi zote zinatimizwa. njia mpya za
uchumi zinavumbuliwa maana watalamu wapo. mkondo mpya wa kuibua maendeleo
unatakiwa kupatikana, vivyo hivyo unapaswa kuelewa kuwa anayesababisha vyama
vya upinzani kupata la kusema ni chama tawala chenyewe.
CCM ikijikita kwenye
shughuli za kutimiza maazimio yake kwa wananchi, sidhani kama ni vibaya. MTAJI
KISIASA, inawezekana hata Mheshimiwa mbunge wa Nzega alipokemea kuhusu
uchimbaji madini na kuhimiza watu kugoma ni MTAJI PIA. Sijui wanasiasa wetu
wanatafsiri namna gani juu ya mtaji wa kisiasa. Na kugoma ilikuwa hatua ya
mwisho pale Nzega mjini Tabora ili serikali isikilize kilio cha wachimbaji wadogo wa madini. MUHIMU; CCM timizeni mliyokusudia kwa maendeleo ya wananchi.
do it all utaona kama akina sisi huku pembeni kama tutakosoa. Ni faida kwenu na
kwa wananchi sisi.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako