Jackline Mluge, Finland |
Na Jackline
Mluge, Finland
WANAWAKE VIPI?
katika ulingo wa ndondi kuna raundi 1 hadi 12. zamani wakati raundi moja kwenda
nyingine inapokwisha, kuna wanaume walikuwa wamevishwa suti au mavazi safi
kutangaza raundi inayokuja ni ya ngapi.
SIKU hizi WANAWAKE wanatumika kutangaza
raundi huku wakiwa wamevishwa vichupi, au mavazi ambayo yanaonyesha nusu uchi
kabisa, wanatembea kwa mikogo sana. Nini hicho?
Hapa bongo utaona WANAWAKE
wanavaa visuluwali vya mazoezi na kugeza kuwa mtoko wa siku, wanasema fasheni.
Kila sehemu ya mwili huonekana, kama minyama au kiuno maridadi na kadhalika.
WANAWAKE mnajidhalilisha ama? naendelea ....
Sasa hivi
wanawake wanafanya kazi zote ambazo wanaume wanafanya. Ilikuwa zamani lakini si
kwa sasa ila wanaume ndio wanao ji dhalilisha kwa sasa unakuta dumezima lina
baka mtoto.Mimi na pingana kabisa haki sawa kwa jinsia zote
simpenzi wa
nguo fupi lakini nadhani kila mtu ana uhuru wa kuvaa anachotaka hiyo siyo kujidhalilisha.
Na kuhusu kujiuza kuna wanaume wanajiuza kwa akina mama wenye pesa tena
wanapanga mstari unachagua kama nguo, na sasa wanawake wanajibadilisha kuwa
wanaume na wanaume wanajibadilisha kuwa wanawake. Hao wanafunzi wanaojiuza
wamezoea kujiuza sisababu hawajapata mkopo- mfano nasoma chuo cha Afya napata
hela kidogo kutoka serikalini lakini muda wangu wa ziada nafanya kazi ya fani
ninayosomea au hata nyingine kujipatia hela za matumizi na wakati huohuo na
soma.
Naamini unapokuwa chuo si mtoto tena umefikia umri wa kujitegemea
kiamawazo lakini nia aibu mtu mzima kufundishwa kuacha umalaya, Hebu niambie
wakimaliza chuo wasipopata kazi watalalamika kazi hakuna ngoja tuendelee
kujiuza.
Limenisikitisha sana kuona watu wenye elimu bado wanakili za kulalamika
kitu fulani badala ya kuchagua njia mbadala ya kutatua matatizo yao mfano
mnaweza kuanzisha kuuza sambusa hostel unajipatia pesa tatizo la wasomi wa
Tanzania mtu akifika chuo hataki kufanya kazi mbaya mbaya anataka kufanya kazi
hiyo hiyo aliyosomea huku kuna watu wanasomea uanasheria au uganga nk lakini
utakuta wanafanya kazi ya kuuza baa kipindi wanasoma wakijipatia hela za
kujikimi na mtu aoni aibu.Tanzania ehiii amka sasa acheni porojo.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako