Daniel Gingo |
Nayaandika haya nikiwa katika ardhi ambayo usalama wa raia
wake umejaa mashaka sana. Ni katika ardhi ambayo Dr. Ulimboka alitekwa na
kuteswa vibaya, ni katika ardhi ambayo kabla hatujasahau ya Ulimboka Mwandishi
wa Habari Daud Mwangosi alikufa kifo cha Kikatili kuwahi kukiona duniani, na
wakati tunaendelea kuwa wenye mashaka juu ya jambo hilo Mhariri Absalomu
Kibanda alitendwa aliyotendwa.
Na hawa ni wale ambao wanajulikana, hatujui wakina kajamba
nani wangapi wametendwa yapi! Naandika nikiwa nayajua hayo!!
Ikitokea kuandika kwangu kukapelekea wahusika kunichukia na
kuniondoa duniani, basi heri waniue lakini ukweli usimame, na kama nitatoweka
ninyi mtakaobaki simameni na kweli hii!
Nakiandikia Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania, chini ya
Mwenyekiti wake Jakaya Mrisho Kikwete, chini ya Katibu Mkuu Adullahman Kinana,
Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula, na Katibu Itikadi na Uenezi Nape Moses
Nnauye. NARUDIA TENA, KAMA NITADHURIKA KWA KUUSEMA UKWELI HUU BASI MTAKAOBAKI
SIMAMENI KA KWELI HII.
Wanafiki na Wazandiki watakataka kujipendekeza ili siku zao
zisonge mbele watasema ninaichukia CCM, wataongeza na kusema ninachukia Rais
Kikwete. Waache wafikiri hivi, lakini ukweli nitausema leo!
MIGOGORO YA KIDINI inayoendelea hapa nchini ni zao la mbegu
ambayo CCM ilipanda katika uchaguzi mkuu uliopita. Kama kuna watu wanauana na
kuchukiana sasa hivi kwa misingi ya kidini, CCM chini ya uongozi wake wote
hauwezi kukwepa lawama hizi.
Walipokuwa wakitumia dini katika kutafutia kura walidhani ni
jambo rahisi sana, walionywa lakini wao wakadhani wanaikomoa CHADEMA.
UDINI tunaoushuhudia sasa hivi hapa nchini CCM inahusika.
Wana mambo mawili ya kufanya kama tiba, nami nitayaeleza:
1. Waungame kuwa kweli walihusika
2. Watubu (waache kutumia udini kutafuta uhalali wa kutawala,
kwa sababu madhara yake ni kwetu sisi tusio watawala.
Noeni panga, chongeni mawe, andaeni silaha zote kama
mnadhani kuusema ukweli huu kutanistahili adhabu, lakini nasisitiza CCM ITUBU
DHAMBI HII AMBAYO WATANZANIA SASA WANAYAONA MADHARA YAKE!
Kwa mkono wangu mwenyewe
Daniel Gingo
Dar es Salaam - Tanzania.
Karibu Nyasa kazi yako nzuri saaana, kaza buti Mpangala. Jukumu ni moja tu, kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi inayoridhisha. Vichua uozo, elekeza na bashiri mazuri kwa kutumia yale yaliyopita na halihalisi ya sasa. Nduguyo Juma Nyumayo, Songea
ReplyDelete