May 30, 2013

ONYO KWA MBUNGE WA JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI(NYASA)


Na Emmanuel G. Ndembeka, Dar es Salaam
 Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri wa MUungano wa Tanzania,1977 inasema kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

HIVYO BASI nami ninatumia uhuru huo kutoa maoni yangu!!!Infact nimesikia juu ya Kikao cha watu wa nyumbani kitakachofanyika Msimbazi Centre.Kwa kweli nilifurahi sana niliposikia motive behind ila naona pia tuwe 

Makini sana na nani atakuwa MGENI RASMI!!!Ningependa awepo mtu asiyekuwa na makundi ya kisiasa ndani yake, lakini pia asiwe ni yule mwenye kujisafishia njia ya Urais mwaka 2015.Mtu wa namna hiyo hatufai kwani mwisho wa siku atatufitinisha afu tuonekane wanyasa ni wanafiki kwa makundi yatakayokuwa yamejengeka ndani yetu!!!!

Lakini pia kama atakuwepo huyo Mgeni rasmi Je sie wadau tumeshirikishwa ili nasi tutoe maoni yetu?Maana nawaogopa sana WANASIASA. Wengi wao hawako kwa ajili ya wananchi ila wapo kwa ajili ya kujitengenezea njia zao ili wazidi kuwa na matumbo makubwa, na wale wasio nayo wanapenda yaongezeke!!!!NIMEMALIZA.SIJAMTUKANA MTU!!!!

2 comments:

  1. Ndugu Mpangala, blogu yako ni nzuri sana na inanikumbusha mengi ya mbinga na Nyasa. Jee? unaijua email ya huyu mdau Emanuel Ndembeka?Sielewi kama anawajua Agatha, Mercy na John Ndembeka toka Mbamba Bay ambao nilisoma nao pale Mbinga in the 70s. Mimi naitwa Athanas, nipo hapa Marekani.

    ReplyDelete
  2. Athanasi nasikitika ujunbe wako nimeupata too late,email yangu Ni gideima101@hotmail.com. Hao uliowataja Ni ndugu zangu wa damu kabisa,kwa bahati mbaya Mercy amefariki miaka 23 iliyopita,Mie Ni mdogo wao

    ReplyDelete

Maoni yako