Na Vitus Matembo,
Mbamba Bay
Leo kilio changu kipo
katika kijiji cha Dar Pori au jina jingine Runyeli. Ambako ni maarufu sana kwa
machimbo ya madini. Hali ya maisha huko ni ya juu sana ukilinganisha na maeneo
mengne wilayani Nyasa.
Maisha yapo juu ila huduma
muhimu hakuna HOSPITALI, Usafiri na Kituo cha POLISI. Kijiji kipo kilomita
8 kuingia Msumbiji, sasa wakazi wa Dar Pori wanalindwaje?
Wakiumwa hupelekwa Zahanati
ya Mpepo iliyopo kilomita 20 toka kijiji cha Dar Pori. Kijiji hicho kina
takribani watu 6000 wengi kuliko hata wakazi wa Mbamba Bay na Liuli, ila watoto
wanaokwenda shule ya msingi ni wachache sana, kwa mfano waliofanya mtihani wa
darasa la 7 mwaka huu ni 11 tu.
Sambamba na hayo yote,hebu
tujiulize WANYASA wenzangu mapato yanayopatikana katka machimbo ya kijiji cha
Dar Pori yakwenda wapi?,
Mpaka sasa hakuna geti lolote
la ukaguzi wa bidhaa na malighafi zinazoingia na kutoka katika eneo hilo? Pia
wakazi wa maeneo ya Tingi, Kingerikiti na Dar Pori kila kitu hutegemea kutoka Mbinga
na si wilaya ya Nyasa, Je tutapata chochote ?
Halmashauri yetu
itafute namna ya kukusanya mapato yatokanayo na machimbo yaliyopo kijiji cha
Dar Pori.
"PAMOJA TUIJENGE
NYASA"
Asante kwa taarifa, ingawa inaumiza roho. Picha zinavutia.
ReplyDelete