Na Vitus
Matembo, Mbamba Bay
Wilaya
Nyasa imeendelea kushuhudia mipango ya maendeleo baada ya asasi ya kiraia
iitwayo Tanzania Agricultural & Livestock Promotion Association (TALIPA) kupewa
kibali na serikali kuhudumia na kuhamasisha wananchi wa Nyasa juu ya ufugaji wa
Kuku.
Taasisi
hiyo inahamasisha Wanyasa kufuga kuku kwa wingi wakipatiwa matibabu na
kuhudumiwa kwa miaka mitatu mfululizo. Inaonesha kwamba kwa kuku mmoja unaweza
kupata sh.1,444,000/= kwa mwaka. Kuku hawatakufa kwa kideli wala tatizo lolote.
Hivyo
gharama ya kujiunga ni sh.15,000/= kwa kila mfugaji ili kupewa Semina na Huduma
bure ya kuku wako. Hivyo TALIPA inashirikiana na kaya katika kufuga Kuku wa
Kienyeji.
Hilo
limefanyiwa tafiti na kuonekana kwamba kwa kuku mmoja atataga mayai 10 na
kutotoa kwa kila miezi miwili. 20% watakufa ambapo watabaki vifaranga 8, ambapo
baada ya miezi 6 , kuku mizao miwili kwa jumla ya kuku 16 na mama kuku mmoja
watataga mayai takribani 17*8. Hvyo gharama ya chini ya kuku mmoja ni sh.
7000/= ambapo mara hao kuku zaidi ya 200 utapata faida hiyo.
NB:
Mazingira na usafi ni muhimu ili kupata kuku wengi zaidi.
TUNAOMBWA
TUSHIRIKIANE NAO ILI KUONDOA UMASKINI KWETU NYASA.
Kwa
mawasiliano piga simu na:0717554488
No comments:
Post a Comment
Maoni yako