Tunajaribu kuhamasishana tena na tena. Kwa walio tayari na wasikie neno hili ambalo lilishaletwa hapa mara nyingi. Tunahitaji kuwa na jukwaa (Forum) ya kuhamasisha na kuchangia maendeleo ya shule yetu.
Ni dhahiri kuwa wengine tumesoma zaidi ya shule moja na tunajisikia vibaya kuona kuwa kwingineko tumeweza na tunajitahidi kuchangia (binafsi ni mmoja wa waanzilishi wa Lundo Sec School nilisoma kati ya 1990~1993 lakini kabla nilisoma pia Maposeni Sec ~Peramiho na Songea Boys High School ~Songea 1994~96)
Huko kwengine tunashiriki
kwenye maendeleo. Naona badala ya kulalamika kuhusu kukosekana kwa ushawishi wa
maendeleo kwetu, naona ni vyema tukazidi kuhimizana. Tusiache asili. Wanetu
watatucheka sana..
Naomba wenye nia ya dhani
watuunge mkono kwa kuonyesha u tayari wao hapa lakini pia wanitumie nambari zao
za simu na anwani za barua pepe (email addresses) kupitia ujumbe (inbox) au
hapa kama hawatajali ili na wengine wazipate.
Kwa wale watakao kuwa tayari
tutawaunganisha kwenye "Group chat kupitia WhatsApp" (kwa yule aliye
kwenye utaratibu huo wa mawasiliano).
Tutakuwa pia na " YAHOO
GROUP EMAILS" Kwa wale ambao nina hakika walisoma Lundo Sekondari,
tutaanza kuuliza mtu mmoja mmoja anaguswa kiasi gani na maendeleo ya shule
aliyotokea. Sina shaka wapo waliotayari kwa maendeleo.
Naomba wengine kama William
Mpangala, James Zotto, John Chipaika, Stephen Maluka. Mateso Nindi, Enock
Ndunguru, Loyce Ntale, Joyce Silimu, Frank Zoto George De Enrico Timothy na wengine
tusaidiane kuhamishana ili hii hoja isipeperuke tena.
Tukipata idadi ya kutosha
tutapanga utaratibu wa kukutana. Itapendeza tukiweza kuchangi kwa kuleza pia
Lundo ulipita mwaka gani kama ulisoma hapo.
"LUNDO SECONDARY
SCHOOL-S0592" https://uk.groups.yahoo.com/neo/groups/lundosec/links/all.
Ni group huru kwa kila anaeguswa na maendeleo. Kwa wale wanaoguswa, wanaweza
kutuma taarifa zao (Nambari ya simu, mwaka wa masomo kwa waliosoma hapo na
email). Wanaweza kutuma hapa au kupitia anwani yangu ya barua pepe
mandepog@gmail.com au simu 0754375056 (ipo kwenye whatsApp pia. Pia kwa urahisi
wa kuunganishwa tuma kwa email ya group ambayo ni:lundosec@yahoogroups.co.uk.
Tutawaongeza katika kundi hilo wale walio tayari.
Tuna andaa pia
"Directory" kwa wote ambao walisoma Lundo na wale wanaoguswa na
agenda hii. Tunatambua changamoto ni nyingi kwa kila mmoja wetu, ila
tukishirikiana kwa nia moja na kuacha masuala ya siasa (malalamiko) kwenye
maendeleo tutafanikisha. Shukrani
Nakaribisha maoni yenu.
©Imetolewa na George Mandepo,
2014.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako