October 14, 2014

LIULI STAR NI STORI YA MJINI SONGEA



Na Raymond Ndomba, Songea
 
Timu ya soka ya Liuli (LIULI STAR) imetupa raha wapenzi wa kabumbu tuliopo Songea na Mkoani Ruvuma kwa ujumla baada wa kuweza kushika nafasi ya kwanza katika kundi lao. 

Timu hiyo yenye vijana chipkizi, waliojawa na akili na umbile la soka wameshika nafasi hiyo baada ya kuzifunga timu kongwe na zenye wachezaji wazoefu, wenye majina makubwa songea na wanao jiita watoto wa mjini. 

Kati ya mechi sita ambazo Liuli Star walicheza wamefanikiwa kushinda michezo minne (4) na kutao droo michezo miwili. Liuli star ilifanikiwa kuifunga Tigo bao moja bila majibu na magereza ambao ndio washindi wa pili bao mbili kavu.

Pamoja na timu nyingine za hapa songea zilizo shiriki katika kundi hili lakini Tigo na Magereza ndizo timu nzuri na zenye wapenzi wengi katika manispaa hii. Mashujaa hawa toka Nyasa wamekamilisha mechi yao ya mwisho leo mchana kwa kutoka droo na Bomba Mbili United, pia, katika kundi hili mechi zote zimekamilika jioni ya leo kwa mchezo kati ya wapinzani Tigo na Maafande wa magereza; mchezo ambao ulimalizika kwa kufungana bao moja kwa moja hatimae Maafande kufanikiwa kusonga mbele.


Kwa hiyo, Liuli star ni moja kati ya timu sita zitakazo chuana hapo baadae ili kupata timu za kuingia daraja la pili. Michuano hii ipo katika viwanja vitatu tofauti. Kuna kundi la Mbinga, Tunduru na Songea. 

Hongereni Liuli Star kwa kuutumia vizuri uwanja wa majimaji na kutuwakirisha vema wana Nyasa. Tunawaomba wapenzi wa soka na wananyasa waliopo songea na nje ya songea tuwasapoti vijana hawa ili mwisho wa siku waingie ligi kuu

No comments:

Post a Comment

Maoni yako