September 27, 2017

ADHABU KWA MWENDESHA BAISKELI




Jana mchana mwendesha Baiskeli alipita kwa kasi katika makutano ya barabara ya Bibi Mohammed na Morogoro bila kuruhusiwa na taa za kuongoza magari. Wakati anapiga taa zilionyesha magari yapite, na yalikuwa yakipita kwa mwendo kasi mno, kiasi kwamba ingetokea gari linalopita basi angegongwa na kusababisha matatizo makubwa.


Wakati akivuka eneo hilo upande wa pili alikuwepo askari wa barabarani ambaye alikuwa ameinamia simu yake kana kwamba hafuatilii kinachotokea kwenye eneo la kuvukia lenye mistari ya pundamilia. Baada ya mwendesha baiskeli huyo kuvuka, askari aliona ni kitendo cha hatari kwa kijana huyo, hivyo akamkamata upesi. Adhabu aliyompa ni kutoa upepo wote kwenye tairi la nyuma la baiskeli, hali iliyofanya kijana huyo aduwazwe. 

Askari alichukua uamuzi sahihi kumlinda mwendesha baiskeli na kuonyesha funzo kwa wengine wanaohatarisha maisha yao. Kijana huyo aliondoka kimya kimya huku akikokota baiskeli yake.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako