MOSCOW, URUSI
MIKAKATI
ya serikali ya Urusi kuifanya China kama mshirika thabiti na muhimu kiuchumi
umechochea kukuza sekta ya biashara na kufikisha asilimia 22 katika mapato
yake.
Gazeti
la The Moscow Times limesema kuwa ushirikiana wa karibu baina ya Urusi na China
umechangia kuimarisha mapato katika biashara na kufikia kiasi cha dola bilioni
80 mwaka huu huku matarajio yakiwa ni kufikiwa dola bilioni 200.
Taarifa
zinasema kuwa ili kuongeza mapato zaidi China imepanga kuweka mfumo mpya wa
sheria za fedha wenye lengo la kurahisisha mikataba ya kibiashara kati yake na
Urusi pamoja na kuongeza umuhimu wa matumizi ya Yuan duniani.
Takwimu
zilizotolewa na serikali ya China Oktoba 13 mwaka huu zinaonyesha kuwa katika
kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu biashara kati yake na Urusi imeongezeka kwa asilimia 22.4 ambayo ni kiasi cha fedha cha dola za
kimarekani bilioni 61.4. Katika
kipindi hicho hicho, usafirishaji wa bidhaa za Chinja kwenda Urusi umeongezeka kwa
asilimia 17 ambacho ni kiasi cha fedha cha dola za kimarekani bilioni 31.4,
wakati bidhaa za kutoka Urusi kwenda China zimeongezeka kwa asilimia 28.5
ambayo ni kiasi cha fedha cha dola za kimarekani bilioni 30 katika kipindi
hicho hicho.
Aidha,
imeelezwa kuwa katika kipindi cha mwezi Septemba biashara kati ya nchi hizo
mbili zilifikisha dola za kimarekani bilioni 7.6, ambapo thamani ya bidhaa za
China zilizopelekwa Urusi ni dola za kimarekani bilioni 3.79, wakati bidhaa za
Urusi zilizopelekwa nchini China zimefikisha thamani ya dola za kimarekani
bilioni 3.81.
Kiwango
cha ushirikiano wa kibiashara kati ya China Urusi kwa mwaka 2016 kilipanda
kutoka asilimia 2.2 sawa na dola za kimarekani bilioni 69.5. nchi hizo
zimetajwa pia kuwa washirika wazuri wa masuala ya kijeshi na diplomasia.
Biashara
kati ya China na Urusi ilifikisha kiasi cha dola za kimarekani bilioni 5 na
bilioni 8 miaka 1990, lakini kumekuwa na ongezeko kuanzia wakati huo.
Malengo
ya awali ya nchi hizo mbili yalikuwa ni kufikisha kiasi cha dola za kimarekani
bilioni 100 kabla ya kukumbwa na mdororo wa uchumi mwaka 2008.
Takwimu
hizo zinaonyesha kuwa malengo ya Urusi yapo mbali sana ukilinganisha nay ale ya
Umoja wa Ulaya ambako biashara imekuwa ikiyumba miongoni mwa wanachama. Wakati
ushirikiano wa kibiashara kati ya Urusi na China ukizidi kuimarika, hali
imekuwa mbaya kwa nchi zilizopo kwenye Umoja wa Ulaya (EU).Biashara
kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya imeshuka kutoka Euro bilioni 330 mwaka 2014
hadi Euro bilioni 228 kwa mwaka 2016, huku wataalamu wa uchumi watabiri
kuporomoka zaidi.
Hilo
lina maana kukua kwa biashara kati ya Urusi na China kumesababisha kuporomoka
kwa biashara ya EU na Urusi. China inatarajiwa kuchukua nafasi ya EU kuwa
mshirika muhimu wa kibiashara kati yake na Urusi ifikapo mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako