NA.HONORIUS
MPANGALA
INASADIKIKA
Polisi wa China walikuwa wanacheza mchezo uliitwa 'Tsh-u' ikiwa na maana ya
piga mpira. Mchezo huo ulipenyeza Japan na maeneo mengine ya Roma.
Soka
lilingia Uingereza mwaka 1066 wakati wa utawala wa Mfalme William. Kutokana na
wachezajj wengi kupata matatizo ya vifo mfalme Edward na wengine kama Richard
walipiga marufuku na kutoka kauli ambayo Kwa yoyote atakayehusika au kuonekana
anacheza soka atenda jela.
Mwaka
1848 ulifanyika mkutano katika chuo cha Cambridge na kutengeneza sheria 17 na
kutumia maeneo yote ya Uingereza.Moja ya sheria ilikuwa kuruaha mpira ulirushwa
Kwa mkono mmoja yaani 'throw- in'.
Klabu
ya Sheffield Fc ndiyo ya kwanza kuanzishwa. Ilianzishwa mwaka 1855 ikiwa na
katiba na sheria za Cambridge. Mchezo
wa kwanza kuchezwa ilikuwa kati ya Sheffield fc dhidi ya wapinzani wao na
watazamaji walikuwa ni 600.
Charles
Aldo ndiye alikuja kuufanya mchezo wa soka kuwa wa kusimimua pale alipoanzisha
mashindano Kwa vulabu mwaka 1871. Na klabu ya wanderers ikachukua ubingwa huo
huku mchezo ukihudhuriwa na watazamaji 2000 waliolipa kiingilio cha paundi moja
Kwa kila mtazamaji.
Ni
Charles Aldo aliyefanya mpango wa kuandaa pambano la kwanza la kimataifa mwaka
1877. Ilikuwa kati ya Scotland dhidi ya England na matokeo ya mechi hiyo kuwa
sare tasa(0-0) Ndio maana hadi sasa mechi za Scotland na England huwa ma
msisimko baina yao Kwa kiasi kikubwa sana.
Mwaka
huo wa 1877 ndio sheria ya kutumia dakika 90 ilianza kutumika.Pia katika goli
uliwekwa mtambaa panya 'crossbar' badala ya kamba. Pia waamuzi wanaochezesha
mechi kutokutoka katika timu zinazocheza yaani uwepo wa mahusiano kati ya
mwamuzi na timu inayocheza.
Katika
maamuzi awali sheria zilikuwa katika vitabu hivyo walicheza na pale
ilipoonekana ni kosa mechi ilisimama na walikimbilia kufunua kitabu na kutazama
sheria inasemaje na kufanya maamuzi.Na waliita Reference book na baadae ndo
sheria zote ziliamuliwa na maamuzi Kwa kumwita referee wakilitohoa toka kwenye
reference.
Klabu
ya Preston Ndiyo ya kwanza kunyakua ubingwa wa ligi ya Uingereza mwaka 1888
ilipoanzishwa.Na sheria ya uwapo wa wachezaji wa kulipwa ilianzishwa. Misri
ndio nchi ya kwanza kushiriki kombe la dunia kutoka bara la Afrika. Ilishiriki
Kwa Mara ya kwanza 1934.
Yawezekana
uliyajua ila nilikuwa nayakumbusha tu. Sasa nakuacha na maswali la
kiuamuzi.Kama wewe ni mwamuzi wa soka wakati unachezesha mpira, mchezaji
akamrudishia mpira golikipa wake na akaudaka ndani ya eneo la golikipa dhahiri
atakauwa golikipa atakuwa amefanya kosa. Je ni adhabu gani utakayoitoa?
Je
unajua kwanini magolikipa wengi baada ya kuudaka mpira huwa wanapenda
kuudundisha unajua maana yake kwanini wanadundisha mpira?
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako