November 15, 2017

WANAFUNZI 21 WA SHULE YA ST. PAUL LIULI WANASHIKILIWA NA POLISI KWA UHALIFU.

NA MWANDISHI WETU, LIULI
 LEO wanafunzi 21 wa kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ST. PAUL LIULI iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamefanya fujo kwa kuharibu miundo mbinu ya shule kama kuvunja vioo vya madirisha kwa kushinikiza mwanafunzi mwenzao aachiwe baada ya kukamatwa na Simu shuleni hapo. Baada ya ukaguzi kwenye mabweni yao, wanafunzi hao walikamatwa wakiwa na vipisi vya bangi, vifaa vyenye ncha kali ikiwemo visu na Panga. Mkuu wa Wilaya ameagiza sheria zifuatwe kwa Bodi ya Shule kukaa, kupitia na kutoa adhabu kwa wanafunzi HAO kutokana na Makosa yao.

Chanzo:ITV


1 comment:

Maoni yako