January 04, 2018

ZAWADI YA MWAKA MPYA 2018! KITABU

Adella
ADELLA ABELL ni mtani wangu. Jirani yangu nyumbani. Sahibu wangu. Dada yangu. Ni msomaji mzuri wa vitabu. Katika kuanza mwaka mpya amenipatia zawadi ya kitabu hiki chenye masimulizi ya visa, mikasa, kesi,upelelezi na hukumu mbalimbali zilizowahi kutolewa na mahakama ndani na nje.
Mojawapo ya mkasa uliomo kitabu ni ule wa familia ya George Liundi, mkewe Doris Liundi na watoto wao (Nadhani wengine wamewahi kusikia masimulizi ya maisha ya Taji Liundi).
Awali nilipanga kupumzika hadi Januari 10 ndipo nianze kusoma kitabu. Lakini Adella Abell amefuta ratiba hiyo kwa zawadi maridhawa. Tamaa imenizaba kofi, nimeshindwa kujizuwia. Zawadi hii nimeitia mikononi saa 11 jioni na kuanza kuisoma saa moja usiku wa Leo. Nimefanikiwa kusoma kesi 5 katika kitabu hiki chenye jumla ya kurasa 300. Ni matumaini yangu baada ya majukumu mengine nitakihutimisha Alhamis saa 5 usiku.
Kwa hakika ninamshukuru sana msomaji mwenzangu kuthamini maarifa. Zawadi hii ni kubwa kwangu na inafaa kuigwa na wengine kuwafanyia rafiki zao. Natambua wapo wanaonunuliana vitabu, lakini wengine hawajafanya. Hatujachelewa, muda tunao. Heri ya mwaka mpya 2018.
Asante sana jirani na rafiki yangu Adella.

©Markus Mpangala
Januari 3/2018
Dasalamu

No comments:

Post a Comment

Maoni yako