August 31, 2007

Barua Ya Sekunde Moja

Jana nilikuwa karibu naandika ujumbe kwa watu mbali mtandaoni,lakini nakuambia nilistajabu mtu ninayemwandikia alikuwa kakaa karibu na kompyuta yake bwana naye akaanza kujibu hapo hapo wakati mimi nilikuwa naamini naandika barua ili nijibiwe kama ilivvyo posta mara anuani,kulamba stempu,kushika wino,kununua karatasi n.k

Acha bwana Fred Macha akajibu hapo hapo,ee nikashangaa mzee wangu kumbe yupo nami muda huu toka London.yaani kaacha kulicharaza gita halafu anapiga gumzo hapa? Gumzo hilo si lile la kulonga kimahaba "chat" katika mtandao bali unaandika barua kama unamwandikia baba,mama,kaka,dada,binamu n.k huku ukikaa miezi sita au wiki kadhaa kusubiri majibu,lakini jana nikajibiwa kwa sekunde moja.Yaani ilikuwa saa moja na dakika tano usiku halafu kanifahamisha kwamba yeye pale London ni saa 11 jioni yaani walikuwa wajidai mitaani tu huku wabongo tunajificha ndani kuogopa wakora...kisha kuamka siku inayofuata kwenda kutafuta mkate.

acha kabisa barua za sekunde moja hizi