August 24, 2007

Kushushwa hadhi maana yake nini?

Hivi kuna hekima gani kudai haki ya kushushwa hadhi hapa ulimwenguni?kwanini tunazungumzia kushushwa hadhi katika masuala muhimu ya nchi?
Utakuta kiongozi au raia fulani akidai kwamba ameshushwa hadhi..halafu anaidai hadhi hiyo kama kitu chochote mano wa pipi au kijiko h asukari.

Kama kuna anayebisha basi awatazame viranja wetu kule kijiweni kwao Dodoma,awatazame walivyo na nyuso kama yuda kwa kudai kwamba wameshushwa hadhi,hivi sijui hadhi ni mdudu gani huyu.Halafu hoja kuu inageuka mkuki kwa nguruwe na huku shangwe zikimiminika kama wachanganyaji wa saruji sehemu za ujenzi.

Hivi kuna kifo hochote ukikosa hadhi? kwani hadhi maana yake nini?kwani kuna hadhi inayolindwa na sheria za nchi hii?.Sitaki ushahidi hapa ila viranja wetu ni kama wako chekehea au kama kanbi za mahujaji maana ni porojo na uwongo mwingi ndio ajenda za siku zote.
Amka kijana,nhi imevamiwa na wakimbizi wazaliwa wa nhi yenyewe.

5 comments:

 1. poa ndugu lazima wapate freshi ya shamba

  ReplyDelete
 2. maana yake kutunza matumbo yao ili waendelee kutafuna pia ili wewe ukae hukohuko kijijini kwenu ukinuaka mihogo na pumba za mahindi na kahawa maana mbinga huko kuna wamatengo na wanyasa pia.lakini unajionyesha umebobea katika uvuvi kwahiyo ili wasishushwe hadhi ni lazima wajionyeshe kujua jua.

  ReplyDelete
 3. poa bwana,kama hujui ni kwamba wanataka hata wale wenye biashara ya machinga waondoke kisha wabaki wao ili wakija wakoloni waone kweli nchi imeendelea kwa kujenga viota kama vya ndege.vipi huko uliko ni salama kama wakaazi wa mijini walalama hivi.

  ReplyDelete
 4. yaani inatia uchungu na hasira,binafsi naogopa sana huu ukimya wa wananchi ipo siku waktaona imetosha

  ReplyDelete
 5. pasua anga pamoja na uchanga wa blogu hii nimeona na naju huu ni mwanzo.nimesoma fikra zako mwanzoni mwa blogu nimekubali sana hoja yako ya kuwatazama watu wanaotulilia

  ReplyDelete

Maoni yako