August 24, 2007

Unampenda nani...

Wako watu wanaosemekana wanampenda mungu wao na wako tayari kufanya lolote kwa ajili ya mungu huyo.Wanabeba tabasamu wakati mwingine utadhani mungu kawaambia kwamba ni wao pekee watakao uona ufalme wake(sijui uko wapi).

Jambo la ajabu watu haohao wanaweza hata kuchukia ndugu zao na kumpenda mungu wasiyemuona eti kwamba yeye anaouwezo wa kumwona yoyote.Wanatenga binadamu wenzao kwa misingi ya imani zao,itikadi zao juu ya dini.Uadui unakuwa mkubwa kwasababu wanamtetea mungu ambaye hata siku moja hajaweza kuwaambia wamtetee.

Hoja kuu hapa ni kwanini watu wanaweza kumpenda sana mungu halafu wanahukia hata ndugu zao waliozaliwa nao tumbo moja?Mungu atawapa thawabu kwa kuonyesha jeuri na ujivuni kwamba wanazo imani tosha? binadamu tunapaswa kupendana bila itikadi za imani za dini au vinginevyo tunahitaji kuwa katika njia moja ya kuombeana lakini utakuta madhehebu mbalimbali yanahuburi ujinga na kuwalisha waumini wake ujuha tu.
amani na upendo kwa wote bila kujali imani ya dini ni muhimu sana kwa binadamu

1 comment:

  1. poa kaka naona mambo yako siku hizi,lakini polepole ndio mwendo

    ReplyDelete

Maoni yako