August 29, 2007

Tunadharau kiswahili..

Niliposoma makala inayozungumzia kiswahili katika gazeti moja leo hii baada ya kuingia toka kijijini Lundu,nilikuta natamani kutwanga ngumi ukutani,nilahamanika ile mbaya kwani nikaona watu wote hapa wilayani Mbinga kama vimulimuli.Makala inazungumzia namna Watanzania tunakidharau na kuona kiswahili kama lugha isiyo ya kisomi,ya kishenzi,mbovu,haina maana n.k

Lakini ukitazama hao wanaojiita wasomi eti kwa kuwa wanajua maneno kadhaa ya lugha ya kikoloni ni majuha na watumwa namba moja kuliko wale wasiosoma hapa ulimwenguni.Kwani utawakuta wakiamini eti Kiingereza ni lugha ya kuwasiliana! heee sasa kiswahili ni lugha ya kufanya nini nyiwe watumwa?,Usomi gani hata matumizi ya lugha yenyewe yanwashinda halafu muwe wajivuni?

Wengine hata sarufi maumbo,miundo,na matamshi hawajui matokeo yake hujifanya eti wanashindwa kuongea vyema kiswahili au nini sijui huko, yaani ******** hamna adabu kabisa hivi mnafikiri usomi ni kuja kiingereza na kubetuanetua midomo kama joji kichaka? mlaani***tena mpotee kabisa.

Usomi gani wa kuwa mambumbumbu wa wa lugha yako ya asili,usomi gani huu kama si mauaji ya fikra.Ndio maana tunasema kwamba eti wasomi wa siku hizi hakuna kitu,hivi mnadhani ni nini kama si hiyo lugha yenu ya midabwada.Wengine eti hujifanya kuongea na kuchanganya maneno ya kiingereza na kiswahili.Hilo nasema mko*** kabisa,mtaendelea na utumwa huku wenzenu wakitamani lugha hii ingekuwa yao maana wanaiendeleza sana.