August 29, 2007

Acheni Dhihaka

Kama hasira ni mbaya basi bora ziendane na tukio halisi,na kamwe siwezi kuacha hasira za na uchungu moyoni kama TUPAC SHAKUR,BOB MARLEY,J.K NYERERE n.k kwani kama watu hawa walipigani kuondoa unyonge wetu,halafu sisi kwa kujifanya kuja tunakaribisha tena unyonge ambao wenzetu walipigani uondolewe.

Yaani hatuna jeuri kabisa,kila kukicha eti lazima kuongea kiingereza au kuheshimu lugha hiyo kwa kuwa ya kimataifa,hivi mataiafa gani?.Ninaposoma vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya kiswahili nafarijika na kujihoji kwamba hivi wanaojifanya wasomi leo mbona hata msamiati mmoja wa kiswahili hawajui?Ilikuwaje Biblia ikatafsiriwa kwa kiswahili na kueleweka namna ile?

Mbona kamusi yetu ina maneno mengi tu yanayoashoria kwamba tuko zama sahihi ikiwa tutaamua kutumia lugha yetu? kwani maneno mengi ya kiingereza mbona yanatokana na lugha ya ya kikabila iliyozungumzwa zamani ya kibritaini pale visiwani uingereza halafu leo tunasema ya kimataifa na kimawasiliano.Kwani kiswahili si lugha ya kimawasiliano,acheni dhihaka nyie ****** wana wa kizazi cha wajivuni mbona wazee wetu waliamini miaka hii ndiyo ya kuruhusu lugha yeu kwani wakati ule walibanwa nbavu na hao wanaofanana na rangi ya ngozi ya nguru****?

Hisia toka moyoni;wakati ndio huu.Daahhh! nilitamani kutwanga ngumi mtumbwi wa mvuvi mmoja juzi baada ya kujidai anayajua maneno ya akina blea.lakini nikaona hii mbaya nikatulia na ghadhabu zangu na kumwambia acha dhihaka ndugu yangu mbona Wachina wanaongea kikwao na wanafanikiwa?