September 03, 2007

Jumatatu hii ninaanza na hasira

Kuna jamaa wanapenda sana kuchezea muada wa watu.Lakini ukiwaambia kwa lugha ya kikoloni kwamba "Mastering;Time Management"wanadhani jamaa anajidai eti kasoma..sivyo ila ni lazima kuzingatia muda wako la sivyo utajikuta kila kitu harijojo.

Ndio maana mwanablogu freddy macha anasema kuna watu hawana nidhamu hususani sisi vijana.Yaaani hata salamu hakuna,ndio utamaduni wawapi huu,unatokea wapi huu eeeh.

Lakini siku ya leo nimeanza kwa kupotezewa muda na watu wasio kanuni maana wanaishi kama wapo hekaluni wakati hata huko hekaluni kuna kanuni sasa hivi jamaa linanipigia simu sijui nini wakati anajua wazi kuwa hapa kwa wanyasa ni mvumo waziwa tupu.Kama sauti kubwa basi ujue kuna ngoma mahala tena utasikia watu wanasema kuna kipaimara na ukatakumeni n.k
sijui kuishi bila kuwa kanuni na miiko inakuwaje hivi wenzangu mnasemaje hilo

1 comment:

  1. Kwa kawaida kuanza wiki kwa hasira zenye kipimo chake ni vema sana kuliko kuwa na hasira za jumla.ila ni jukumu letu kuwa na hasira za maaarifa si a chuki

    ReplyDelete

Maoni yako