September 05, 2007

Tanzanite Inaitajirisha India!

Tanzanite inachimbwa Tanzania na inapatikana hapa pekee,lakini habari toka India zinaseama madini hayo yamewezesha ujenzi wa viwanda 15 nchini humo.Viwanda hivyo vinajihusisha na uchongaji,utengenezaji wa bidhaa zinazohusu madini pamoja na usambazaji dunia kote!!!!!

Kitabu cha orodha ya makampuni cha India kinaeleza kuwa makampuni hayo yapo katika miji ya Jaipur,Jimbo la Rajastham nchini humo.Majina ya makampuni hayo ni Gems,Pankas Gems,Sumati Gems,Daga Gems,Vidhan Gems na Ghoshi Export n.k yaani ayko mengi mno kifupi ni hayo.

Najua utashangaa nimepata wapi wakati hapa kwetu Nyasa habari tunategemea Redio za Malawi,Redio za Tanzania ambazo ni chache tu.Lakini habari hii nimeiona leo hapa Mbinga mjini bwana maana leo nilipania kuja mjini kujionea shughuli za walioelimika.Acha tuendelee kuvua samaki huku tukidumisha utamaduni wa nidhamu.Yaani nimestaajabu hata ikirejea nyumbani Yule mzee wangu(baba) mwenye hasira na kutowaendeleza wananchi sijui atasemaje.

Lakini hali hii si njema kwani hata Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki aliwahi kuwaambia wasomi wetu pale chuo kikuu Mlimani 'waone soni'kwani madini hayo yanainufaisha sana nchi yake.Hii niliambiwa na rafiki yangu wa palepale,hivyo usishangae kuwa kwangu kijijini LUNDU hapa nikashindwa kujua huko mjini mnafanya nini.
Jamani mimi napata mfumuko wa hewa(pulesha) maana hali hii si njema.
uhuru daima amka mwana wa Tanzania,wakati ni huu

4 comments:

 1. ndugu zangu ni kwanini hatuwezi kunufaika na madini hayo?mbona ni mali yetu watanzania?hivi viongozi wetu ni wajinga au wanafiki?tuamke sasa tujikomboe

  ReplyDelete
 2. haya mateso yataisha lini?lakini mbona nawe hujatoa suluhisho unalaumu tu? tusaidiane

  ReplyDelete
 3. haya mateso yataisha lini?lakini mbona nawe hujatoa suluhisho unalaumu tu? tusaidiane

  ReplyDelete
 4. nashindwa kusema ndio maana nimewaachia wasomaji muamue kuhusu hatima ya nchi yetu

  ReplyDelete

Maoni yako