March 19, 2008

Machi Mwaka 2002;Yasinta Kwanini,kisa kinaendelea.

Nimerudi na kisa kileee kinachonihusu pengine zaidi ya kunihusu na kinawahusu wengine,mimi sijui.Hebu ngoja nikiandike tena hapa maana siyo mimi labda wengine kinawahusu.Mwezi machi 2002,Yasinta katoroka kwao,kamkimbia baba,mama na nduguze,wala hataki kusema anakokwenda.Nyumbani wazazi wanashangaa mwenetu tumpendaye kaondoka bila kuaga ni maajabu hayo.Yasinta katua Mbinga mjini,katulia stendi na raifikiye Vumilia wanapiga soga za hapa na pale lakini hatimaye mnyasa anatokea,ana-afro, katweta ghafla anajiuliza huyu binti vipi?Haya soga za hapa na pale wanakumbushana na mnyasa enzi wakiwa shule,lakini mnyasa anauliza kulikoni upo hapa? mara ghafla Yasinta anaomba "tafadhali ukiulizwa kuhusu kuniona mimi{yeye}usiseme".Mnyasa anashangaa kumbe binti katoroka nyumbani kumfuata mpenzi?Jamani kupenda tabu,mapenzi ni kikohozi kuficha huwezi aliimba Fresh Jumbe.Binti amependa hataki shule hataki kusikia maonyo ya wazazi,masikio kaziba pamba,mahaba yamekolea, lakini kwakuwa mnyasa anamjua vema akasaili hee mwenzangu nimesikia hutaki shule kulikoni?Sipewi jibu, nazungushwa huku na huko binti anajiona kumaliza kidato ni mwisho hakuna tena hamu ya shule kisa mapenzi mmh.Mwishowe mnyasa anashauri vipi uahirishe safari,looh.. akaambiwa alipe nauli aliyolipia tiketi kisha awezekuahirisha safari,mnyasa akaduwaa akasema huyu siku hizi kawa mbogo wa mapenzi.Lakini kwani mnyasa akawa anajua hapa anapenda lakini kwa mtindo huu acha ajifanye hana hizo hela,unajua shilingi ngapi?Watu wa Mbinga wanajua wakati huo nauli mpaka makao yetu makuu Songea ni....samahani sitasema.Binti anasafiri anakwenda kuonana na mpenzi wake,waubani wake, mwandani wake,yaani ampendaye.Mmh wapi bwana yako wapi hayo mapenzi mathubuti?kuna kuacha shule tena?Mbona yupo huko.......kwenye baridi anasoma,sijui kwa ari au ndiyo wasomi wetu wa siku hizi.Kifupi alicharukia mapenzi,akaona ganda la mua la jana........na masikitiko ya mnyasa kwa kuwa alimpenda basi katoa kauli za kulaani na bado zinamtesa,yako wapi mbona bado kasheshe inaendelea?Maisha ya Lundo yalikuwa ni simulizi murua.Ngoja nikomee hapa kwa leo.

2 comments:

  1. markus mpangala06 April, 2008

    Mapenzi ni kitu cha ajabu sana kwani wapo watu wanaoamini kwamba huwezi kuishi bila fulani kwa kuwa unampenda aua kumhitaji sana.kama kweli kupendana ni mwisho wa safari ya mapenzi kwanini watu wajiue kwakuwa wameudhiwa na wapenzi wao.Kila mtu anaye mtu aliyewahi kumpenda katika maisha yake,pengine hata wewe msomaji kuna mtu alikufanyia mambo ya kihuni.Lakini naamini kwamba wanaolalamika kwamba wnatendwa vibaya na wapenzi wao waongo kwani kutendwa ni wewe kushindwa kujielewa hivyo kuiharibu nafsi yako kwa kusingizia umetendwa.ukiwa na imani thabiti juu yako huwezi kulalalmikia kutendwa au naongopa?

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mapenzi ni kitu cha ajabu na kweli kuna watu wanaweza hata kujiua kwa sababu ya mapenzi. Nadhani hii ni nature yaani kumpenda mtu mpaka kiasi kwamba hata kama ukiolewa au ukiwa na mtu mwingine hutaweza kumsahau yule wa kwanza.

    ReplyDelete

Maoni yako