March 23, 2008

Shamrashamra,Vifijo,Shangwe na Mbwembwe za Wanyasa

Jana nilikuwa na wanyasa hapa kijijini kwetu,jambo la kwanza nililojiuliza ni je wanyasa watakula nini au watasherekea vipi sikukuu hii ya pasaka kwa wakristo.Nikawafuata wazee wa mila wajuao desturi na tamaduni zetu ili wanipe mbwembwe na shamrashamra za kale kwa wanyasa.Nikaambiwa nyakati hizi kwa vijana ni hatari sana kwani mengi ambayo kale hayakuwapo yapo,hivyo shangwe hizo ziendane na kujihadhari japo kidogo.Zamani wazee wetu walikuwa wakitayarisha samaki kwa ajili ya wanyasa waishio mijini ili wakija kupumzika kwao waone kweli wapo nyasa,lakini kipindi hiki ile hali ya kujali imepungua na chanzo ni kubadilika kwa mfumo wa maisha ya mwanadamu.Basi unaambiwa wanyasa wanacharaza ngoma za Lendeku,madogori na nyingine nyingi,vijana walichangamka jana wakasahau machungu ya kulima nyakati hizi.watoto wanarukaruka kwa mikogo kuifurahia sikukuu hii,wamebeba virugu vya kutwanga wenzao{kama mchezo fulani hivi},wazee wanasema vijana wa siku hizi hawajiamini kama kale.Naambiwa vipi kujumuika kuselebuka mimi naulizia hayo mambo,nikajibu ni moja ya kusherekea pia kwani napata nasaha za wazee wa jadi wenye kila aina ya thawabu.Basi unaambiwa kuku wakienyeji wamechinjwa{hakuna kuku wa kisasa huku},mbuzi,ng'ombe na wengine waliwinda sungura na wanyama wengine kwa ajili ya kitoweo,hizi ni nyakati za wanyasa kusahau samaki kidogo na ugali wao wa muhogo lakini lazima samaki awepo ili kukamilisha unyasa wetu.Watu wamejazana wanafurahi sana jumamosi yenyewe kabla ya jumapili.Ni porojo za hapa na pale yaani kila mnyasa ni furaha tupu,mungu awalinde wanyasa wenzangu hawa.ngoja nikomee hapa kwa leo.

2 comments:

  1. Markus umenikumbusha mbali sana madogoli lindeko nk. ama kweli hii ndio pasaka maana bila ngoma na kurukaruka basi sherehe. ndio kama ulivyosema hata kuwe na nyama lazima kuwe na samakina kaugali ka muhogo kidogo. mnyasa ni mnyasa
    Ila um esahau kusema walic heza lizombe pia.

    ReplyDelete
  2. markus mpangala06 April, 2008

    ni siku ya mwokozi wala usijali ni maisha hayo ya kuamini ukombozi wa watu wote

    ReplyDelete

Maoni yako