March 29, 2008

Wanyasa wangali wakiselebuka na Nyakati maalumu

Amini usiamini,utake usitake wanyasa ni wanadamu wanaofahamu namna ya kuzitumia hizi nyakati maalumu.Hawasiti kuselebuka kwa raha zao huku wakipiga ngoma za Lindeko,Madogoli n.k lakini kuna jambo nilisahau wakati naandika hapa kuhusu shamrashamra hizo,kuna aina fulani ya ngoma nilizisahau lakini kwa bahati mbaya,lakini nimekumbushwa na dadangu wa blogu ya Ruhuwiko{ngoja nitaandika ili uisome blogu yake},kanikumbusha Lizombe,Muhambo wa wamatengo,nami dakika hii nakumbuka Chomanga,mganda,makanya,sindo n.k
Kwa sasa huku Nyasa ni kama nyakati maalumu zipo kila siku kwani watu tunaselebuka kwa raha na kusahau uchungu fulani wa maisha{bila shaka unajua namaanisha nini}.Huku watu wajipa likizo isiyo na malipo,wanakunywa pombe zao za asili komoni,lihutapahi,mbege,chimpumu ya wamatengo na hizi zinazozalishwa huko mjini kifupi hazina soko hapa nyasa hazitakiwi.Basi jumapili ya pasaka yenyewe watu wamependeza,wafurahia siku hiyo,wanatabasamu hapa na pale wanakumbushana pasaka ya miaka iliyopita n.kWatu wanakumbuka mambo mengi ya kitamaduni ambayo yanawafanya waone fahali kuzaliwa na kuishi nyasa.Yaani mambo bado yanaendelea hapa watu hatujapumzika na wala nilipoibukia pale Mbinga sikapenda kukaa sana nikarudi nyasa ili nijionee furaha hizi.Siyo siri dadangu pale Sweden amekumbuka mengi anakosa nyakati hizi kwa wanyasa.Hii ndiyo nyasa watu wanajimwaga mitaani.Lakini kikubwa unywaji wa pombe hizi mjini hutumia mishkaki lakini hapa watu kama kawaida yao samaki maarufu kwa jina la "Kapili" yaani ni kama 'kachumbari' ya pombe kwa walevi na wanywaji .Samaki hawa wanakuwa wamekwisha kuchomwa na kukaushwa vyema basi inakuwa utamu juu ya utamu na pilipili pembeni yake.Wasiolewa kazi yao kukumbushana na kujadili maisha n.k kina dada wanajumuika kupiga gumzo na kina kaka maana ni nyakati maalumu hizi huja mara chache.Watu wanafurahia maisha acha wajifurahie

3 comments:

  1. kwa kweli umeniacha hoi kabisa yaani hizo ngoma zote ulizozitaji nazikosa sana. yaani sio uongo nazikosa sana nyakati hizi. pia hiyo kapili hiyo. Kweli kabisa watu huishi mara moja tu.

    ReplyDelete
  2. vipi bwana siku hizi watu wameacha kupika/kunywa myakaya?

    ReplyDelete
  3. kuburudika ni sehemu ya maisha kwani hayo ndiyo yanakamilihs mzunguko wa dunia,bila kuburudika huwezi kukamilisha au kuchangamsha mwili na tunaweza kukufungulia mashtaka kama hutaki kufurahi au mnabisha..{natania}

    ReplyDelete

Maoni yako