June 26, 2008

Ndesanjo Macha na Fred Macha Karibuni Nyasa

Hivi mnajua utamu wa dagaa wa ziwa nyasa?Hamjawahi kula?Mnagoja nini?Sijui niseme nini,kama mashtaka nipo tayari kuzikwa hai kutetea nyasa.Nilikuwa najiuliza hawa jamaa{baba zangu} niwakaribishe vipi,nilikuwa nahoji kwanini Mwalimu wangu wa blogu hajanisapoti toka nimwambie nimeanza kublogu?Nikajiuliza mbona siku hizi hajibu hata waraka pepe wangu?Lakini alisema mambo mengi huwa anazidiwa nitamsamehe.Lakini sijawahi kumwambia mzee wangu Fred kama ninablogu yangu,halafu juni 12 mwaka huu pale kwa Weshi Lema TPH nimenunua kitabu chake kile kinaitwaje?...Ebu dada Yasinta nikumbushe hapo Sweden hujapata?aaaah kinaitwa MPE MANENO YAKE.Kuna visa vitamu sana kwenye hiki kitabu.Sasa nikajiuliza nifanye nini mimi mvuvi wakati kila siku nabanwa na ratiba za kuvua dagaa,mandongo,kambale,mbelele,vituwi,ngorokoro,pelege n.k nitaweza kuwasiliana na wazee wangu hawa?Mmmh kwanza yule mzee Fred siku hizi amebadilisha anuani yake sijui kwanini au wanamghasi wale majambazi wa mtandaoni?Ndesanjo naye kila siku warsha,makongamano, juzi pale nimemwona kwenye ile dokumentari nilipoenda pale Mbinga mjini{mwenzenu kublogu mpaka nifike mbinga}.Sasa nitamwambia nini au nilalamike kama wale wezi wa richmondi na yule mzee mamvi anayejidai kulilia 'natural justice' samahni nilitajiwa hilo neno hata sijui sheria mimi.Basi ni hivi karibuni nyasa wazee wangu Ndesanjo Macha na Fred Macha mle dagaa kama hawa...tunawaandalia ugali wa muhogo....mtamu sana...

4 comments:

  1. mhhhh kabla wa hao wazee wako hawajakujibu kama watafika au vipi mimi nasema bila kukuribishwa nafika kwani ugali wa muhugo na dagaa....mtamu sana. Umesahau kuwa ambia pia mbufu, magege na pia mbasa. mie nilishasahau kama kuna samaki anaitwa vindongo

    ReplyDelete
  2. Wewe Jirani,

    Nimefurahi sana kukupata leo maana nilikuwa sijui kama kuna kijiwe safi kama hiki ambacho kuna vitu vizuri na vinavyoendana na wakati kama hivi.
    Ic yaani nikirudi Tanzania tu tuwasiliane ili niwe na vacation hapo Nyasa kwani I can't wait kula dagaa na ugali wa muhogo.

    Kazi yako ni makini na naamini utatizimiza ndoto zako za kuwa mwanafalsafa, upo makini na unaburudisha sana.
    Tuwasiliane

    Mbilinyi

    ReplyDelete
  3. Anonymous29 June, 2008

    Kaka Mbilinyi asante sana kwa maoni yako karibu tena mara nyingine.Unajua nilikuwa najiuliza hivi naburudisha au siwezi?Lakini sikuwahi kujua hilo toka Mwalimu wangu Ndesanjo aniambie Blogu siyo upepo wa kupita zingatia,sasa naelewa vyema hakuna kulala tunasonga kwa mwendo wa karatasi ama kinyonga.

    Karubuni nyasa wote,asante kaka Mbilinyi

    ReplyDelete
  4. Kaka Mpangala,

    Nakuonea wivu sana ulivyosema leo utaogelea kushinda bata, hiyo ndo raha ya kuwazaliwa ziwani.
    Nikiwa home (Njombe) huwa nawaza lini niende ziwa Nyasa.
    Tunahitaji picha nyingi sana kutoka ziwani naamini tunaweza kutangaza utalii pia kwani kanda za nyanda za juu kusini imesahaulika sana ingawa bado tuna nafasi ya kuitangaza na watu kama ninyi ndo mnashikilia mizizi kuhakikisha kizazi kipya kinatoa habari muhimu zinazohusu nyanda za juu kusini ulimwengu ujue.
    Asante sana na nafarijika na kazi yako.

    Lazarus Mbilinyi
    Ontario - Canada

    ReplyDelete

Maoni yako