July 30, 2008

Nisemavyo mnyasa leo

Ngoja leo nijikumbushe kuandika kama nilivyokuwa awali.Unajua nilikuwa naandika tu bila kuweka picha hapa kijijini?Kilichonifanya niandike tena ni kuona watu wana akili za mseto.Nikikwambia watu wanaakili za mseto ujue hakika zimejichanganya zile zenye uvundo,uozo na zile zenye hekima za kudunduliza.Kwanini watu hawataki kuamini kwamba uwezo wao ni fimbo ya maisha?Kuna sababu gani watu kulilia peremende yenye mchanga?Ni hivi sijui leo nikasirishwa au ninawaza nini lakini naona ninachoandika hakieleweki.Labda nimechanganyikiwa.Acha bwana waenze zao huko wasitake kunighasi mnyasa miye kwani wananini,hawaniwezi navua samaki sana tu.Kuna sababu ya kumghasi mtu katika maisha yake?Ngoja,ni hivi natumia muda mwingi kupambana kuendeleza msingi wa maisha lakini najikuta nataka kukwama eti sababu naona fulani kapendeza au nahisi ana maisha maridadi,jamani huu upungwani nimeuvaa hapa leo hakika hata sijui naandika nini. Hivi nimejieleza vizuri au sieleweki hata kidogo?Mmmh labda nimechanganyikiwa kwani leo nahisi hali tofauti.ngoja nikapumzike kidogo pale ufukweni labda nitapata wazo zuri baadaye.aaaaaah nimekumbuka,hivi kuna sababu ya mimi kulazimisha kuwa kama wengine mfano maisha,itikadi,itifaki,falsafa na mengineyo?.Umenielewa?ngoja bado aaaah acha nipumzike kwanza

2 comments:

 1. Kaka,
  Mimi nimekuelewa na naamini umfikia hatua nzuri zaidi kujiuliza na kujiona kama vile umechanganyikiwa naamini kila mmoja wetu kuna wakati hupata hali kama hiyo.
  Kitu cha msingi mimi naamini wewe una uwezo mkubwa sana kiasi kwamba unaweza kufanya zaidi ya hao unaona wamefanya vizuri kuliko wao.
  'All hard work brings a profit but merely talk leads to poverty" Najua wewe ni mtu mwenye juhudi sana hivyo ipo siku utakuwa tofauti na hao unahisi wamekuzidi na wanapendeza.
  Brother, You can be anything you want, if anybody alse can do it, am sure you can do it better. Uwezo unao na ni suala la kuweka malengo na kuyafanyia kazi bila kuangalia nini kinatokea kwenye crowd.
  God did not make any person, race, nationality to be inferior or superior but by deciding ourselves from inside our mind.
  Nina imani miaka 5 ijayo utakuwa mbali sana na Mungu atakusaidia.
  Keep on going!

  ReplyDelete
 2. vipi kaka mpangala ni kitu/ au mambo gani hasa yanakufanya uchanganyikiwe au kuna mtu anakuchanganya. Kwa nini?

  ReplyDelete

Maoni yako