July 08, 2008

Siyo Ukali Bali Anafurahia Nyasa

Kuna swali dadangu Ruhuwiko bloguni aliniuliza kuhusu huyu mnyama,nilikwepa kulijibu shauri nilikuwa natafuta kwanza picha yake na sasa nimeibamba.Ilikuwa adhuhuri fulani watu wakakusanyika kushangaa huyu mnyama wengine wakajiuliza ni Mamba gani huyu asiyejificha?Lakini ukweli ni kwamba dadangu alikuja nyasa toka ughaibuni lakini akaogopa kuogelea kisa mamba.Kimsingi huyu ni mnyama ambaye anaogopwa sana na Binadamu.Pale Liuli mzungu mmoja aliitwa Rainer alishikwa kwenye jicho na mamba mpaka kifo kikamkuta ikadaiwa ni sayansi ya kiafrika.Mimi sijui ila kwa hakika mambo wapo lakini kusema ndiyo hatari katika ziwa letu ni hapana,hawa ni wanyama ambao kila mmoja anatamani kuwaona,niambie kama unaogopa nikupe mbinu za kupuuza na kukupa nyakati za kuibuka kwa mamba ziwa nyasa.Kwa faida ya wasomaji ni kwamba nyakati za masika ni rahisi sana,hususani mwezi desemba na machi.Pia kiangazi hasa mwezi oktoba jua kali na joto kali,mamba hutokea sana vipindi hivi lakini siyo kuhatarisha maisha....hivi nimejitahidi kujibu au sijaweza?.....

1 comment:

  1. usinidanganye bwana. halafu kwanini huyo mamba akamate jichoni sio kichwa kizima au mguu haieleweki nakuomba ufafanua zaidi

    ReplyDelete

Maoni yako