August 04, 2008

gumzo,michapo na mseto

nashangaa hata sijui nataka kuandika nini lakini najikuta nataka kuandika.Ngoja kwanza,kuna kitu kinanifurahisha sana halafu sikijui sawasawa lakini najiona nina furaha toka jana niliofanya.Haa utashangaa eti sikijui huku nakifanya-ngoja ni hivi nahisi naandika lakini sijui naadika nini ambacho wanyasa wenzeangu wanafurahia. Nilikuwa mbinga juzi bwana nikaona jinsi watani wangu wamatengo wanavyochakarikia samaki,yaani wanahaha wananunua pale karibu na kituo cha mabasi katika soko la samaki.Aise niliwaona wanahangaika na kusukumana kisa kitoweo toka nyasa.Hivi najieleza vizuri kweli?unanielewa mnyasa mwenzangu?Nimekumbuka tena wenzenu huku nyasa sasa ni kula mpuchulela/kisamvu,kuoposha mandongo/kula mlenda,chaina bila kusahau mangatongo/eti wengine waita mbegu za upupu kazi kwenu.Huu ni msimu wa samaki kupotea shauri ya kuogopa kwisha(natania)naona kila mtu anahaha kupata japo kidogo mpuchulela.Mmh ni hivi nimepata kitabu kile cha 'makuadi wa soko huria' kiliandikwa na porofesa/profesa chachage chachage.unajua wanyasa kuatmka profesa ni kazi nzito sana?wao huita porofesa au yule osama wanaita usama/hosama.Unaielewa au nianze upya?Nahisi sijui kujieleza vizuri sijui nimepagawa na nini lakini najua kitabu hiki kinanikuna sana nasoma hadi maandishi yafutike yote.Mmm ngoja hivi kuna sababu ya watu kublogu?aah bora uniue kabisa kuliko kunizuia kublogu aise patachimbika yaani hapatoshi na mwendo wa kutunisha misuli tu. Ngoja nikomee hapa na michapo ya mseto

7 comments:

  1. Hakika hicho kitabu inaonekana ni kizuri sana je huwezi kunitumia na mimi kwani inaonyesha umefurahi sana ni kweli sababu ni hiyo tu au kuna kitu kingine kinakupa raha?

    ReplyDelete
  2. kusoma vitabu raha ndugu yangu usifikirie hapa nyasa nyasa kazi yetu ni kuvua tu samaki...hapana hata kusoma vitabu vyenye simulizi nzuri au kusikiliza ile stesheni ya Malawi simulizi za kale za mababu ni tamu sana karibu

    ReplyDelete
  3. Najua umenikumbusha sana wakati nilikuw mdogo babu na bibi walipenda sana kutusimulia hadithi tena palepale ilipo shule yako ya sekondary utamu sana je nitapata kitabu hicho au

    ReplyDelete
  4. unaweza kukipata,lakini toa oda yako nikuunganishie. Kina itwa 'Makuadi wa soko huria'. kiliandikwa na yule Profesa niliyeweka picha zake hapa bloguni.
    tuma anuani zako nikutumie kama unahitaji kweli

    ReplyDelete
  5. kina husu nini hicho kitabu?

    ReplyDelete
  6. Kinahusu namna ubepari unashangiliwa na makuadi wake bila kujua siri,sheria na kanuni zake.Kuna mahaba ya mseto,utamu wa lugha,falsafa na kuifikirisha akili,maisha ya wa duni,namna matajiri wanavyotumia mwanya wa kuwapora masikini kwa kisingizio cha msaada,namna viongozi wetu walikosa falsafa na itikadi. chanzo chake ni pale utawala wa mkapa ulipotaka kuleta 'uwizishaji'ubinafsishaji katika mradi wa kufuga kamba pale rufiji huku makamu wa rais na helkopta yake akitua kuhakiki.Yaani kwa kitabu hiki ndiyo maana mkapa hakumpenda sana mwandishi wa kitabu hiki na alimchukia daima mpaka kifo kilipomkuta akiwa mkutanoni kule kibaha.Alikuwa profesa wa Mlimani katika siasa.Kitabu kiwanashambulia akina mkapa na ujuha na uroho wao. mmmm najua uatasema nimeanza siasa.nikutumie au

    ReplyDelete
  7. Ni kweli umeanza siasa kwa hiyo umeshaeleza kinahusu nini tayari nimeshaelewa. Asante

    ReplyDelete

Maoni yako