August 09, 2008

Ni upendeleo au nini jamani....aa wapi

nimeamua kujipendelea ndugu yangu.Wahenga walinena raha jipe mwenyewe mwanakwetu.Wacha nijipendelee kwani wao wakiweza wananini hata sisi tushindwe tunanini,wasalimie wote masela wangu TKZee,Mandoza,Mina Nawe kule bondeni kwa Nelson Mandela na midundo yao ya Kwaito inanikuna sana.Mmmh najua dada Yasinta ameshaweka kanda kuanza kucheza Kwaito maana anazipenda mno jasho linamtoka kila siku kunengua kwaito!! aaah wapi raha tu,yote yatimilike ndani ya muda huu,eee bwana muda bado unaruhusu!!Karibuni nyasa

5 comments:

 1. kaka Mpangala huyo dada yako Yasinta inaonekana upo karibu sana naye na inaonekana unalipenda sana jina la Yasinta je huyo dadako Yasinta anaishi wapi huna picha yake na sisi tumwone basi. Hujafanya vibaya kujipendelea kwani watu wanasema jipende kwanza mwenyewe na halafu wengine watakupenda.Msalimie dadako Yasinta

  ReplyDelete
 2. markus mpangala13 August, 2008

  Huyu dadangu ana makeke sana yaani mjanja kama unavyomwona Ronaldinho yule jamaa wa Brazil akiwa dimbani.Huyu dadangu nampenda sana uanajua kwanini? mmm ngoja nimesemaje? hebu? aah ndiyo nampenda sana kwani hana noma anajua kuheshimu wadogo zake wala hajali kwamba umri wake ni wa kujivunia basi nimheshimu....acha yeye wala hana mikogo anapenda sana kuwa simpo yaani nampenda sana namna ananichukulia kama mdogo wake na ananipenda.Hivi ukiwa na ndugu yako anakupenda,anakujali huwezi kumpenda? wewe acha hizo kwani hujui kupenda? mmm nimegundua nyie ndiyo mnaotaka kunikosanisha na dadangu nimpendaye...ngoja kwanza halafu akisoma hapa uataona anaanza kuuliza namaanisha nini... wewe dadangu nakupenda tuuuuuuuuuuuu. ukisoma usimwambie mtu miye simo kesi kubwa hii hapendi mzaha umeiona picha yake ngoja nitakuwekea siku moja...subira yavuta....... mmm ila anakunywa pombe bwana ananiudhi kidogoooooo siyo sana

  ReplyDelete
 3. Aise ningekuwa na kaka/mdogo kama wewe ningejidai sana nakuonea wivu sana. Msalimie dadako basi

  ReplyDelete
 4. markus mpangala14 August, 2008

  tatizo lake ni mipombe na kulewa kulala kilabuni lakini nampenda tuuuuuuu haina noma

  ReplyDelete
 5. Basi unaonekana upendo wako ni wa uongo pole sana na dada yako Yasinta. mpe pole kutoka kwangu pia au nipe namba yake nijaribu kuongea naye.

  ReplyDelete

Maoni yako