August 13, 2008

Kapewa Mwaliko kalala kilabuni

Ninataka kuandika nini? hebu funua kichwa kuna nini? ngoja nikupe mseto wa gumzo mimi napingana sana unywaji pombe,unabisha? nitazame vema.Kuna jamaa kapewa mwaliko wa kuhudhuria kasherehe hapa kwetu.Basi jamaa kauvalia vema,amependeza,uso umenawiri kisa mwaliko umekuwa maridadi kwake. lakini sherehe imekolea watu wanaselebuka jamaa kaanza kutwika pombe,kama wale jamaa zenu wa safari wanasema safari moja huanzisha nyingine.Jamaa kaanza kulewa pombe zimenzingua hana lolote anaropoka huku anayumbayumba. Watu wanashangilia bwana si unajua kusherehekea? Basi jamaa kalewa hata asijue choo kilipo akaazna kujikojolea nguo zimetota pombe ameitwika hana hali.Basi wakamchukua na kudai wanampeleka nyumbani kwake,mmmmm wapi bwana jamaa wakamlaza kwenye kilabu cha pombe za kienyeji,si unanjua wanyasa vilabu vyao yaani mende na wadudu kibao wakaanza kusherekea matapishi yake mdomoni na inzi wakafanya sherehe mdomoni kwake lakini jamaa hajui kitu.Mwaliko huo alipokuja kushtuka yupo kilabuni ikabidi arejee nyumbani.Alipofika akajilaza kitandani..baadaye eti ananiambia yaani simpendi eti nilimwacha kwenye sherehe halafu kalewa. ngoja apate majambozi au vipi watu wangu.Jamaa kapewa mwaliko wa sherehe ya kulima shamba kwa ushirikiano,pombe zimemnogea kalala kilabuni.Inzi wakafanya sherehe mwilini mwake. Inabidi akae na dadangu mmoja hivi anazitwika pombe nasikia naye aliokolewa na majirani zake wakamlaza kwao,we acha tu mwaliko huu....ndiyo maana sitaki pombe miye mnyasa

2 comments:

  1. Inaonekana kuna mtu unayempenda anakunywa sana pombe je? umeongea naye na kumwambia kuwa pombe zinaua Au ndo una unamwacha tu azeeke na afe na akisha kufa au zeeka utajilaumu

    ReplyDelete
  2. markus mpangala14 August, 2008

    huyu jama nikimwambia anasema namwone wivu kwahiyo nimeamua kumwacha anywe azeeke mpaka uso uwe na makwinyazi kama ya yule jamaa wa chama cha Republican MacCain sijui macheni

    ReplyDelete

Maoni yako