October 07, 2008

mbaroni kwa kumbaka mwanafunzi......

na HAPPY KULANGA, SONGEA.
Mkazi wa Mpandangindo mkoani hapa (Ruvuma) Filbert Ndomba(17) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Songea kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 8.
Mwendesha mashtka Inspekta wa Polisi Patrius Mlowe alieleza mbele ya hakimu mkazi Joseph Fovo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo septemba 16 mwaka huu, saa nane mchana, katika maeneo ya Mpandangindo ndani ya manispaa ya Songea mkoani hapa.

Mlowe alidai kuw mshatakiwa alimuingilia kimwili kwa nguvu binti huyo na kusababishia maumivu makali ambayo yalimfanya apige kelele zilizomshtua mwenye nyumba pamoja na wapangaji ambao walikwenda ndani kwa kijana huyo na kumkuta amemvua nguo zote mtoto huyo na kumbaka.

Mshtakiwa amekubali kosa na kudai kuwa mtoto huyo alimfuata chumbani kwake ndipo alipoamua kumbaka. Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo oktoba ambapo hukumu itatolewa. Mshtakiwa alirudishwa rumande.

WAKATI HUOHUO, MBAMBA BAY.
Mkazi wa Mbamba bay Sevelina Komba(34) amefariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki isiyofahamika na kuvunjika miguu. Sevelina alikuwa akitibiwa katika hosptali ya wilaya ya hapa Mbinga, mkoani Ruvuma. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi(Happy Kulanga) mjini hapa,kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Falhum Mshana alisema tukio hilo lilitokea siku ya Idd Mosi, saa nne usiku katika maeneo ya hapa Mbamba bay.

Mshana alisema Sevelina Komba alifariki siku ya pili saa asubuhi katika hospitali ya wilaya Mbinga na kwamba aliymgonga hajafahamika baada ya kukimbilia kusikojulikana. Alisema mwili wa marehemu umezikwa jana na pia Polisi wanaendelea na uchunguzi sambamba na kumtafuta aliyemgonga marehemu huyo.

1 comment:

  1. Jamani sasa vipi hii sasa mbona inatisha hakuna wanawake wa kuoa kubaka watoto wadogo tabia mbaya sana watu kama hawa ni kuwafyeka tu. Maana hata kuoa wasiruhusiwe. Kama mzazi nimeumia sana, Je kuna habari zaidi kama hawa watu wana akili timamu au?

    Na pia mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi. Amena

    ReplyDelete

Maoni yako