September 10, 2009

YASINTA NA JOHARI YA MATUMAINI (2)

YASINTA: we Markus uko wapi, mbona huonekani?

MARKUS: nakja bwana, nipo hapa jirani tu, tulia boli

YASINTA: uko karibu, pouwa nakusubiri basi.

MARKUS: nimeshafika hebu njoo dada yangu nipo hapa....

YASINTA: aaaaaah we dogo umekuja kwa usafiri gani tena?

MARKUS: Bajaj......(kicheko kidogo)

YASINTA: ha ha ha ha ha wewe Bajaj ndiyo nini tena?

MARKUS: huoni hicho kiberenge cha matairi matatu?

YASINTA: poa, lete stori mtu wangu, duh! hii kali, mzee kipara wewe kwanini umenyoa kipara?

MARKUS: aaah bongo joto kipindi hiki we huoni?

ERICK: (anaingilia gumzo) Mmmhh joto sana hapa, kweli

YASINTA: muone Erick utadhani unajua sawa sawa hicho kiswahili.

MARKUS: hee Erick kumbe Rasta? ha ha ha ha LoL

Msomaji unaweza kudhani simuliz fulani hivi kwani kama ujuavyo ZEE LA NYETI ninavyohusudu michapo na gumzo la hapa na pale. Lakini ghafla naona mtu kainamia meza anaandika kitu kwenye daftari nauliza niaje naambiwa naandika post ya leo kwenye blogu. Mi hee haya bwana. Huyu mtu ananipa maswali na mazungumzo yanakolea hapa na pale.

Msomaji mengine fikiria tu mwenyewe wala usisumbuke sana maana nimesitisha kuendelea nayo ili nisiandike mengi na kujiona namfahamu sana huyu mtu.... lakini sasa.... haya ngoja nikomee hapa........... ingawa skupenda kukomea hapo.... KWAHERI KWA LEO.

1 comment:

  1. Chivili lepi cha kujova ujovili goha. Nene hoi ndongu vangu.

    ReplyDelete

Maoni yako