September 15, 2009

NKATA BAY: Bandari salama, lakini.....

Ha ha ha ha ha ha! Nayakumbuka niliyopita hadi kufikia uamuzi wa kuomba mnisamehe niliowakosea. Najua mapitio yale yalikwaza ndiyo maana simulizi ni nyingi hadi zikanifikia.........au vipi Babu? ha ha ha Pouwa ha ha ha ha ha ndiyo maana nimesema sina elimu ya FALAKI! Eeeehh! najua hayanihusu, nisielewe sana bureeeee!!!!!

Nkata Bay ni moja ya bandari iliyopo kaskazini kabisa mwa Malawi, ukiangalia pichani unaona Mv Ilala ikiwa bandarini. Kwa maana hiyo basi unaweza kujenga picha fulani kuwa ni eneo ambalo halina bandari nzuri ama kubwa kama ya Mtwara ama Lindi. Ni kweli, nilifika bandarini hapo kwa mara ya kwanza 1999 na mara ya pili ilikuwa mwaka 2oo1. Wakati huo tuliambiwa marekebisho makubwa yanakuja kwajili ya kuboresha huduma zake.

Hii ilitokana na suala la biashara kati ya TZ na Malawi. Lakini wakti huo kulikuwa na uongozi wa Rais Muluzi ambaye siyo siri aliwapenda na kuwapendelea sana waTZ, hilo lipo wazi kabisaaaaaaa. Lakini baada ya kuingia Rais Bingu wa Mutharika, mwanablogu mahiri tu ingawa ni mwanasiasa nakiongozi wa nchi, upendeleo ule umetoweka na hata wafanya biashara waliokuwa wakitumia sana usafiri wa meli wamepungua kama siyo kwisha.

Mv Ilala ni kubwa sana, kuna wakati kulikuwa na matatizo kwani bidhaa zilikuwa adimu huku meli likiwatia nanga Mbamba Bay ikiwa na mzigo kidogo. Hii yote ni kwasababu ya ujio wa Rais mwanablogu Bingu wa Mutharika. Simlaumu kwa lengo lake la kujenga uzalendo wa nchi yake.

Nkata Bay tatizo lake ni swa na pale bandari ya Manda, kwani kwa mujibu wa wachunguzi inadaiwa kuwa kuna miamba mingi chini ya maji-na sifa yake kubwa ni kina kirefu. Kwa uapnde wa TZ tunaringa kwa kuwa na maziwa mengi, lakini Malawi wanalitumia ziwa hilo kwa umakini sana, ukifika pale bandari ya Chilumba wanavua kwa zana za kisasa, na sheria kuhusu uhai wa samaki unalindwa sana.
Wavuvi wameelimishwa ipasavyo wanaelewa umuhimu wa kutunza mazingira na kuvua samaki bora.

Nkata Bay ni pazuri kama mji na bandari inapswa kuwa nzuri zaidi licha ya uzuri, changamoto kubwa kwetu ni TZ ni kuiboresha bandari ya Mbamba Bay au Liuli maana ile ya Chiwanda tuliambiwa mbali na hakuna kina kirefu, kweli nimeshuhudia hali ile na kuna upepo mkali sana ukielekea kijiji cha Kwambe ambapo ni jirani tu na Chiwanda. Bandari nzuri...lakini Rais Bingu apunguze "kuwafukuza" wabongo...... ila anatufukuza kwa kuwawezesha wamalawi...ndiyo hapo changamoto yetu ilipo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako