September 15, 2009

KARIBUNI NYASA, KARIBUNI SAMAKI

Basi nikamwambia unataka kufahamu chakula nikipendacho zaidi? Hakuna kingine zaidi ya UGALI WA MUHOGO kwa smaki aina ya KAMBALE.... nikaona anacheka,,,, tena kwa harara utadhani amekamata lile jani au ile pombe mashuhuri hapa nyasa ya Myakaya. ha ha ha ha basi nikamkumbusha wale samaki aina ya MAGEGE nikamwambia utaniambia nini masika ifikapo? Nikajikumbusha raha za mji wangu niupendao wa LUNDU, nikamwambia naridhika na kutulia sana nikiwa hapa, nikamweleza zaidi kuwa labda anipeleke MBEYA mahali pengine ninapopapenda zaidi... halafu na pengine ni pale jijini LILONGWE kule kwa asili ya akina MPANGALA, kwa wajomba na mababu zetu, napazimia sana napahusudu sana mahali pale, vipi ile klabu ya soka ya Sivo service United huishangilii wewe?

Mi naihusudu bwana, si unaona ilivyojipangia mikakati? Halafu siku ile pale ulinizome ilipofungwa na MTL Wanderers, we haya tu bwana...... eti akacheka kwa mikogo ati. Ngoja na Mbinga magharibi sasa kuna mchakato wa kuifanya Mbinga magharibi kuwa wilaya rasmi.

Najua watagombania kati ya LIULI, MBAMB BAY na LITUHI wapi waweke makao makuu. Maana hata wiki jana nilikuwa na rafiki yangu kipenzi Raymond Ndomba..... kijana mcheza soka ninayemshangaa.... anaweza kucheza namba yoyote utakayo mpanga uwanjani tangu golikipa hadi winga wa kushoto....lakini shule imemfanya awekeze huko.......na sasa anawania kupata nini kile kinaitwa MASTERS. Huyu alinidokeza kuwa wazo la makao makuu la Wilaya Mbinga magharibi litakuwa shubiri maana kila mji unapenda iwe hivyo...nadhani LIULI wanaweza kupendelewa eti ni katikati ya wilaya yenyewe.

Tuache hayo, twende katika samaki wetu hawa watamu sana na adhimu duniani. Ni nyasa bwana wapi kwingineko utakako pata samaki hawa, ha ha ha ha raha sana. KARIBUNI NYASA, KARIBUNI SANA lakini neno langu siyo sheria au vipi waungwana? Pendaneni kwa mpango!

1 comment:

  1. Somba, somba, mwenge na ugali wa mayao kunoga kweli mpaka utajiuma vidole. Umenikumbusha sana chakula changu. Nakumbuka mwaka juzi nilipokuwa nyumbani nilitembelea kijiji nilichozaliwa sio kingine tena ni LUNDO mjombwa wangu wa vile anajua jinsi nilivyo mroho wa samaki akaenda ziwani na akaja na samaki MAGEGE. Basi naishia hapa....

    ReplyDelete

Maoni yako