February 28, 2010

ALIKUPENDA!

aLIKUPENDA, hUKUMPENDA,
uLIMTENDA, aLIKUPENDA,
hAKUSEMA, aLITENDA,
uLIMTAWALA,aKATEREMKA
mATEKA,uLIMTEKA,

Tantabelua,Hakupenda,
Ulimchosha,Hakutamauka,
Akataka,Hukutaka,
Taashira,Ukamwonesha,

Sununa,Ilimjaa,
Alikupenda,Hukumpenda,

Ukamfanya,Taahira,
Sinema,Kushunga,
Alikufanya Shorewanda,
Malaika Sambamba,

Kumbe Mwanasesere,
Sembuse mkuna Upele,
Punje hukuona Mbele,
Mpyororo kwenda mbele
Alikupenda, hukumpenda.DOKEZO; 'Shorewanda' ni ndege mdogo
                  'Sununa' ni masikitiko
                  'Kushunga' ni kufukuza
                  'mpyororo' ni mdanganyifu
                  'tamauka' ni kuishiwa tamaa
                   'taashira' ni dalili/ishara
                  'tantabelua' ni ghasia.

1 comment:

Maoni yako