February 22, 2010

BARUA YA PAPII KOCHA KWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


SHUKRANI KWA DADA SUBI SABATO, KURUHUSU KUSAMBAZA BARUA HII

Barua ya Papii Kocha kwenda kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 02/21/2010

Barua hii ametumiwa Judith Wambura (Jide) LadyJayDee na ameruhusu itumike katika vyombo vya habari na mawasiliano ila shukrani na taratibu za kunakili zizingatiwe. Tafadhali zingatia hilo.

MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam

Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais

Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.

Mungu akubariki
Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

2 comments:

  1. Markus mwana wa Mpangala,
    Shukrani kwa kuni-linki kwenye blogu yako mkuu. Shukrani sana!

    ReplyDelete

Maoni yako