January 28, 2010

PENDO BANDIA!


Niambie, Pendo Bandia,
Wapi Linapoanzia,
Moyoni au Kichwani?
Huzaliwa Jinsi Gani?
Hulelewa Jinsi Gani?
Nijibu Hima Nijibu!
Nalisubiri Jawabu,
Macho Ndivyo Hulizala
Na Chakula ni Kulola
Na Hufia Pendo Hilo
Pa Pale Penye Malalo
Sote Tupige Malalo
Kwa Kifo Cha Pendo Lile
Ninaanza, Ngoo Ngooo
Ngooo, Ngooo, Ngooo!

KIBWAGIZO
Nahitaji Mwanamke Halisi!
Ni Mwanamke Makini
Sitaki Mwanamke Feki
Nahitaji Mwanamke mimi
Atumie Muda kunifahamu mimi
Sihitaji Mwanamke wa Mahotelini
Ndiyo tiba ya kunipenda mimi.

MAWAZO YA PENDO LILE!
Ulizaliwa Peke Yako,
Kutoka kwa mama yako,
Ni wazi uko peke yako,
Unapaswa kuangalia yako,
Namna gani utaishi kivyako,
Hata kama uko Peke yako
Yote yanawezekana

Iwaze amani
tafakari furaha ni nini?

3 comments:

 1. mwenga kugana naku lihengu kweli Na lihengu zaidi pala pa witakiwa kuwagana wandu wamahele. Lihengu hapa livili....

  ReplyDelete
 2. Vipi Markus kaka,
  kwani limetoweka?
  Ama lakupa mashaka,
  Nahisi wahuzunika,
  Pendo limeshakuteka!

  ReplyDelete
 3. Fadhy Mtanga kaka,
  Januari 20, mwaka jana,
  Safari ya Mbeya, kaka,
  Baada ya Tunda kutoweka,
  Waikumbuka, siku ile,
  Niliyonena pasi simile,

  Nikaibukia jiji lile,
  Kupumzika nitulie
  Basi sikumbushe pendo lile,

  Basi 2010, naikumbuka siku ile,
  Katu kutekwa isiwe,
  Nakumbuka tu pendo lile,
  Pendo bandia, silile.
  pendo bandia, wapi lianzie?

  ReplyDelete

Maoni yako