July 05, 2010

ILIKUWA NASIBU?? iko wapi JUWATA?


Hoja ya Mama Mchungaji Koero Mkundi imenigusa kiasi fulani. Na kwa dhati nampongeza sana kwa kuibua hilo, na inaonyesha namna gani anagusa bongo zetu. Nimejiuliza maswali lukuki kabla ya kuacha maoni katika kibaraza chake. Baada ya kujiuliza nikaongeza,  je INATOSHA?

Je inatosha tu kusema ilikuwa NASIBU au ILIPANGWA? Binafsi NALIPINGA HILO. Kwasababu ukiangalia namna mwenendo ulivyo kuhusu mjumuiko huo unaweza kudhani ilikuwa NASIBU hawa viumbe hai kukutana hapo. Lakini kama mijumuiko mingine haikusemwa, basi huu ulikuwa sehemu tu ya kile kilichowahi kutokea.

Kwangu NASIBU ilikuwa siku nilipokutana na Kamala Luta, pale Regent Estate- mtaa wa Milingotini- Mikocheni katika mgahawa wa vitabu uitwao SOMA(SOMA CAFE). Ile ilikuwa NASIBU kwasababu hapakuwepo taarifa za kukutana kwetu bali warsha za FRED MACHA(toka London-Uingereza) zilitukutanisha.

Tulioona hapakuwa na kufahamiana kwa lolote ndiyo maana Kamala aliniuliza swali ambalo Fred Macha alikuwa akiniuliza mara nyingi kwamba nina uhusiano wa kidugu na Maggid Mjengwa? Jawabu langu ni hapana, sote ni binadamu.

Ndipo nikadadisi huyu aniulizaye ni nani? Naam hapo ni NASIBU. kilichofuata ni Kamala kuniuliza jina, ndipo akataharuki na kutaja jina lake(alitulia). Baada ya hapo ni simulizi. Tukirudi kwa kaka Shaban Kaluse naamini nguvu zake alizounganisha na mtani wangu Fadhy Mtanga a.k.a shemeji mtarajiwa zilikuwa na mpango maalumu. wakati mtani Fadhy alikuwa na kundi alilounganisha, huku Kaluse alikuwa na mpango wa kundi pia kuliweka pamoja.

Jambo la kwanza(kwa mujibu wa Kaluse) huko nyuma waliwahi kujumuika kwa kiasi fulani, lakini haikuwa kipaumbele katika blog zetu. kwahiyo ulipangwa mpango wa kuwakutanisha wanablog hapo. Je walianzaje? hapo ndipo palipo na swali. Ukidodosa zaidi utaona kuwa kuna kitu kinaitwa JUWATA. endapo unakifahamu hiki huwezi kusema NASIBU, kwahiyo JUWATA(jumuiya ya wanablog wa bongo) imeshindwa kazi.

Nasema hivi kushindwa siyo kutowakutanisha wanablog kwani siku hiyo mwenyekiti wake Mtakatifu Kitururu tulikuwa naye hewani. Je ilikuwa NASIBU wakati alishaweka namba za simu katika blog yake kuwa atakuwa bongo katika vipengere vya Moro,Dar,Arusha na Nairobi?

Nayo ilikuwa NASIBU? kama kulikuwa na kusudio la kufanya mjumuiko,basi sikuweza kuwa mbali sana, lakini nilipojulishwa orodha iko Movenpick(mahali ambapo sipapendi wala kupatamani- ubepari mtupu), nikajumuika. Nakiri mimi nilichelewa na nikawachelewesha wengine.

Kwahiyo ukiangalia namna mpango ulivyosukwa wa kusema 'IPO SIKU' ndipo siku hiyo ikatimia, tukawa WATOTO WA BABA MMOJA. Jamani mimi nimehudhuria mjumuiko wa Wanabidii pale Mikocheni lakini nawaambia ipo heshima na malengo, ila siyo NASIBU? ukiwa mbali na ukweli mara nyingi unajenga mashaka.

Lakini ukiwa karibu na ukweli unajenga ukweli '.......AND THE TRUH SHALL SET YOU FREE'. Ninachokusudia ni kulipinga suala la NASIBU. na kama huna mawasiliano ya pembeni ya blog zetu hizi(yaani nje ya blogu) utaona hii ni hadithi za CHARLIE'S WILSON WAR na yale mambo ya LAOS au yale ya SECRET OF THE KINGDOM. Kama wengine wanajumuika pembeni bila kuandikia katika blogu zetu hizi inakuwaje?

Maana endapo umbali wa kushinda unawekewa vikwazo, basi ni rahisi kuandaa kushindwa kwakuwa kunawekewa vikwazo..... Hivyo basi hoja ya Mama Mchungaji ni nzuri, lakini je ipo wapi JUWATA? ni kwanini tunalbo tu bila kujipika tukaiva? JUWATA imekufa kibudu?

Maana ni Christian Bwaya pekee binadamu aliyehoji suala la JUWATA. endapo tungeithamini au kuikumbuka naamini swlai lingeanzia hapo lakini siyo NASIBU. wakati Muhidn Issa Michuzi akihudhuria mkutano wa Diasporra, alisfiwa, nami nilisifu kuthaminiwa huko, lakini cha ajabu tumebweteka tu na kuiacha JUWATA ikioza huku tukiwapongeza wanablog wa Diasporra.

Na wengine tunajua hapo Kenya(Piga Kelele), tunajua na huko Taipei. Yote hayo ni NASIBU? kwasababu kuna mambo ni lazima tujiulize kwa bidii. tublog kwa sababu gani haswa? kabla ya kuanzisha blog yetu tunaifahamu JUWATA? tumeitendea haki jumuiya hii kweli?

Kipi kilianza kati ya JUWATA na WANABIDII? je watushinde hata hawa iRafiki,KIKO, na MAL? nina kiu ya kuuliza mfululizo kwani kwangu NASIBU haipo labda tukubali kuwa JUWATA imekufa, haina nguvu wala haiwezi kufua dafu kwa NYAZODE yetu ya nyasa.

Wakati wengine tunamujumuiko midogo midogo tu tunaamini kuwa sisi ni WATOTO WA BABA mmoja. Au labda mzimu wa kuficha uhalisi wa mtu unasababisha kutoweka kwa thamani ya mtu? ndiyo, maana tunatakiwa kwenda mbali zaidi, tuende maili nyingi na kujiuliza NASIBU ni nini?

Tatizo ni nini hapa hadi JUWATA imepotea na tunafika katika NASIBU? Ni vema wakongwe akina Kitururu,Da Mija Shija, Ndesanjo Macha,Fred Macha,Edo Ndaki,Da' Subi,Kasri la Mwanazuo,Yahya Charahani,Simon Regis,Deus Ngowi,Haki Ngowi,William Shao,Nyasigo na wengine waseme nini kinachoendelea katika JUWATA yetu ili tuondokane na NASIBU. Nawasilisha mheshimiwa mwenyekiti wa JUWATA. Je ilikuwa NASIBU?



2 comments:

  1. Ni kweli maswali magumu. Na kila kitu ulichosema ni kwelikabisa katika jumuisho hilo haikuwepo NASIBU kwani wote mlijua. Haya mie sipo huko kwani sikuwepo..lol

    ReplyDelete
  2. haya ni maswali magumu kiasi fulani kwa kuwa sisi tunataka iaminike ni magumu. lakini wakati mwingine (nikishalewa ulanzi) naamini haya ni maswali mepesi sana kama sisi tutataka yawe mepesi.
    nilipokutana kwa mara ya kwanza na bloggers Chacha na Kaluse jambo hili analolifikiria shemeji mtarajiwa lilinijia akilini.
    lakini nikajikumbusha na busara ya kale, Roma haikujengwa siku moja.
    mimi nadhani (naweza kuwa kinara wa kudhani) upo uhai wa jumuiya, ingawa hatuwezi kuuona kwa macho. kadri siku zinavyokwenda ndivyo blogaz tunavyozidi kuwa karibu tofauti na miaka miwili mitatu iliyopita.
    kwa kufahamiana kwetu, ni namna rahisi ya kuelekea kuwa na umoja wenye nguvu zaidi kuliko ule uliokuwepo (wanasema umeaga dunia kibudu)
    tunayo nia, uwezo na sababu ya kuwa na umoja wenye nguvu kwa blogaz wa Bongo. hii inasaidia sana katika kubadilishana uzoefu wa mambo kadha wa kadha katika maisha ya kublog na mengine kwa ujumla.
    hebu kila mtu ajaribu kujiweka karibu na busara ya Mahatma Ghandhi, aliposema, "you must be the changes, you wish to see in the world."
    kila mmoja kwa nafasi yake ajione ni mtu muhimu zaidi katika kuufanya umoja wetu kuwa na nguvu na uhai mrefu zaidi na zaidi.

    nimeongea mengi shemeji aka mtani.

    alamsiki

    ReplyDelete

Maoni yako