October 31, 2012

SEKONDARI YA MTAKATIFU PAULO YANUFAIKA NA MABADILIKO YA ELIMU WILAYA YA NYASA+OFISI YA MUDA YA MKUU WA WILAYA YA NYASA

Sekondari ya Mtakatifu Paulo(ST PAUL'S) ni maarufu sana katika mji wa Liuli. Ni Sekondari kongwe ambayo mdogo wangu Honorius Ngachipanda alisomea shule hiyo. Hii Nise kondari ambayo imekuwa ikisaidia kuchukua wanafunzi wengi tangu ilipokuwa ikimilikiwa na Kanisa Anglikana. 
Lakini sasa sekondari hiyo inamilikiwa na Serikali baada ya kanisa Anglikana kutoa baraka zate ili kupunguza uendeshaji. St Paul's ni shule yenye historia nzuri katika wilaya ya Nyasa.   
LAKINI ... kwa sasa sekondari hii imefanyiwa ukarabati wa kiwango cha juu zaidi.
PICHA YA CHINI, inaonyesha jengo la Bweni la zamani la sekondari Mtakatifu Paulo.


MONEKANO MPYA SEKONDARI YA MTAKATIFU PAULO LIULI WILAYA YA NYASA.

Picha inaonyesha majengo yenye mwonekano mzuri katika sekondari ya Mtakatifu Paulo mjini Liuli katika wilaya ya Nyasa, baada ya ukarabati. Sekondari hii ni moja ya shule zilizonufaika na harakati za mabadiliko ya elimu wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.


JENGO LA MAABARA KATIKA SEKONDARI YA MTAKATIFU PAULO LIULI. Maabara ni moja ya nyenzo muhimu katika mafanikio ya kielimu kwa wanafunzi.


OFISI YA MUDA YA MKUU WA WILAYA YA NYASA iliyopo mjini MBAMBA BAY kama inavyoonekana pichani.No comments:

Post a Comment

Maoni yako