November 14, 2012

MKEKA HADI MBINGA

Hii ni barabara ya Mbinga kutoka Songea mjini. Barabara hii ilikuwa mbovu kwa muda mrefu, lakini sasa imetengenezwa kwa kiwango cha Lami. Kwa sasa suala la usafiri baina ya miji ya Songea na Mbinga imerahisishwa kutokana utengenezwaji wa Barabara hii kwa kiwango cha Lami ambayo itachangia ukuaji wa uchumi baina ya miji hii. Ujenzi wa Miundombinu kama hii inasaidia sana kukuza biashara na ongezeko la kipato miongoni mwa wananchi ama wafanyabiashara. Shughuli za kiuchumi na fursa mbalimbali zitajitokeza zaidi na kuufanya mji wa Mbinga kukuza uchumi wake maradufu. Maendeleo ni uhai. Na sasa unaweza kusafiri salama kabisa bila makorongo, magema, au vikwazo vingine barabarani. Ni mkeka tu huo hadi Mbinga ukitokea Songea. KARIBUNI KUWEKEZA

1 comment:

  1. Duh! sasa safari za Songea -Mbinga zitakuwa rahisi kweli na umbali utapungua...sitakosa kwenda Mbinga....hii lami ingefika mpaka Lundo ...nawaza tu kwa sauti...

    ReplyDelete

Maoni yako