December 06, 2012

UKATAJI MITI NA UUZAJI ARDHI HOLELA WASHAMIRI MBINGA

Na Robert Hyera, Mbinga

Habari zenu,
Kuna mambo machache tu nataka nikwambieni. Katika wilaya ya Mbinga kuna watu wanamiliki ardhi bila hati miliki za ardhi. Kwa sasa kama hujui kuna wageni ambao wananunua ardhi kwa bei ya chini sana ili baadaye wanufaike.
Ardhi inaporwa na werevu, wenyeji tumebaki mikono mitupu, mbali na hilo leo Mbinga kuna wageni weeeengi ambao wananunua miti na kuchana mbao kwa rahisi sana. Bei ya miti hiyo ni shilingi elfu 11 had 20. 

Mandhari ya Mbinga katika kilimo cha kahawa ambalo ni zao kuu linaloongeza kipato cha wenyeji wa Wilaya hiyo, iliyopo mkoani Ruvuma.

Llakin sehemu nyingine kama Iringa mti huohuo unauzwa elfu 85. Kwa sasa 65% ya miti iliyopandwa zamani yote imekatwa. Kwa kuwa mazingira ndio kila kitu kwa binadamu, nilijaribu kuongea na viongozi wachache nnaowafahamu wakaniambia watachukua hatua lakini hakuna kilichofanyika. 
Sasa hebu tusaidiane nyie wote mnaotoka Mbinga tutafanyaje ili kulinda mazingira? Kwa hili la hati miliki, sisi wenye uelewa tuwaelimishe watu wanaotuzunguka waende ofisi za ardhi za wilaya kwa ajili ya kupata hati miliki za ardhi vinginevyo tutakosa hata sehemu ya kupanda mahindi ya kuchoma.

Oktoba 19, via Facebook

No comments:

Post a Comment

Maoni yako