March 09, 2013

LUNDO SEKONDARI INA HALI MBAYA SANA KIELIMU

Richard Mwanja

Na Richard Mwanja, Dar es Salaam

Tangu kutanagazwa matokeo ya kidato cha nne shule mbalimbali zimekuwa na matokeo mabaya sana. Miongoni mwa shule hizo ni Lundo sekondari ambayo ilikuwa ikisifika kwa ubora wa wahitimu na matokeo mazuri.

Lundo sekondari iliwahi kuweka rekodi ya kufaulu wanafunzi wa kidato cha pili, hivyo hakuna aliyefeli kwa mwaka 1999. Sifa nyingi za shule hii ilikuwa nidhamu na wanafunzi kupenda masomo huku wakikabiliana na hali ya maisha na kuyazoea. 

Wengi waliohitimu hapo wamefanikiwa kuwa watumishi imara na kuzalisha wanamapinduzi wazuri kifikra ambao wanaendelea kusukumu gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Nyasa, na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja taifaletu la Tanzania.

Lakini kwa sasa hali ni tofauti. Licha ya kusifika wakati wa uongozi wa mkuu wa shule Bwan Ndunguru, sasa hali imekuwa mbaya sana. Maskini Lundo Sekondari.......masikini wilaya yetu Nyasa....
Inasikitisha kuona shule ile tuliyosoma, shule ile iliyokuwa kinara kwa ufaulu wa kidato cha nne tangu miaka ile ya 90's hadi mwanzoni mwa 2003.... Leo hii shule ni ya division 4 na 0 tuu.... Kwa mtazamo Wangu kutokana na vile nilivyokuwa nikifuatilia matokeo ya shule hii kwa miaka kadhaa,nimegundua shule imekosa Uongozi....

Samahani kwani huenda nitakuwa nimewagusa wengine moja kwa moja,lakini kwa nini wakati ule wa mzee Ndunguru mambo hayakuwa hivi.... Imeniuma kwa ujumla wa matokeo Kitaifa,lakini nimeumizwa zaidi na matokeo ya shule zetu wilayani Nyasa.... Sitaki kuamini kama Sisi ni Vilaza; Hapana!!

3 comments:

  1. Imenigusa sana ..ukizingatia ilikuwa shule yangu ya kwanza ,,,ya msingi yaani...

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kwa sasa matokeo ni mabaya sana, nadhani ni uongozi mbovu wa shule umechangia matokeo mabaya kama hayo

    ReplyDelete
  3. Mtazamo wangu sio uongozi vijana hawajishughulishi na masomo wapo busy na smart phone ,unakuta muda mwingi wanatumia kuchart,kwani uongozi ndio unaosoma au kufanya mitihani?watoto wazingatie kusoma mambo yatakuwa poa Sana.

    ReplyDelete

Maoni yako