May 20, 2013

JAMES ZOTTO: WANAFUNZI NI WAZEMBE, WAVIVU KUPINDUKIA


Na Markus Mpangala, Dar es Salaam
 
Hatua ya Serikali kufuta matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2012 yamepokelewa kwa hisia tofauti. Baadhi ya wataalamu wa sekta ya elimu wanaona serikali haikuwa makini kufanya uamuzi wa kufuta matokeo hayo, kwa madai uamuzi ulichukuliwa kisiasa zaidi badala ya taalamu. 
Baadhi ya wataalamu wanatetea ufanunuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini, Dk. Ndalichako. Katika baadhi ya mitihani wanafunzi waliandika mashairi ya nyimbo za muziki, wakachora picha za wachezaji mfano Lionel Messi na wengine wakachora picha za filamu za Zombi. 

Hali hii iliwashtua wengi na kuona mwelekeo mbaya wa sekta ya elimu nchini. Pamoja na wazazi kulalamikia hali hiyo bado wameshindwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya watoto wao hivyo kuendelea kuilalamikia serikali. 

“Ni mkanganyiko tu! Serikali inatoa ufafanuzi ambao ukiuchambua unaona hauendani na hasira za Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani, Profesa Rwekaza Mukandala. Baraza limefanya kazi yake kitaalamu, lazima tuheshimu. Ningewaona wa maana sana kama wangekuja na suluhu ya kuondokana na matatizo mabovu.  Viongozi wa sasa walipata elimu bora zamani, lakini leo wanasimamia matokeo machafu, siasa na dini zinatuathiri katika kuiangalia NECTA,” 

Hayo ni maneno mazito ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, James Zotto. Hakuishia hapo, akaongeza kwa kuchambua zaidi uamuzi wa serikali juu ya kubatilisha matokeo hayo. 

James Zotto alitoa mfano muhimu ambao unahusisha baadhi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu ambao waliwahi kuomba kazi, lakini hawkauwa na weledi wa kutosha licha ya kuwa na matokeo mazuri sana katika vyeti vyao. 

“'Msomi mmoja alimaliza Chuo mkoa mmoja wa Kaskazini mwa Tanzania, akaomba kazi katika Idara yetu. Siku ya usaili nikamweleza ataje vitabu vitano alivyosoma katika fani yetu! Lakini cha kushangaza alishindwa kabisa. Nikamkumbusha tafiti za  Walter Rodney, akasema anafahamu. Huwezi amini nilimhoji tena, nikauliza What is the main thesis of  the book? Akashindwa kujibu, nikabaki kushangaa tu, nikajiuliza hivi hii elimu ikoje ambapo mtu ana matokeo mazuri lakini uwezo wake ni mbovu? Nikamuuliza kwa Kiswahili swali jingine, ‘Paradigm'  gani  ambayo Walter Rodney ameandika? Cha ajabu akashindwa kujibu. Sikuchoka, maana nilitaka afahamu umuhimu wa kuielewa fani yake sio matokeo yake kwenye vyeti tu, nikamuuliza kitabu gani anakipenda sana na  kinamvutia? Hakika alishindwa kujibu, ina maana hakuwa akisoma kitabu chochote, huku akijivunia matokeo mazuri kwenye vyeti vyake. Msomi huyo alikuwa GPA ya 4.6.” anasema Zotto.

“Leo hii serikali inafuta matokeo na kuwadekeza wanafunzi wavivu na wazembe kama hawa. Wahitimu Wwengi  laiti kama wangekutana na usaili Upya kabla hata ya kuonesha GPA zao, lazima wanataalamu tuone fedheha sana. Sisi wakati tunasoma tulikuwa tunataabikia katafuta shahada zetu, hawa wanafunzi wa siku hizi wanacheza sana ten asana, na hayo yaanzia huko chini ambako leo wanadekezwa na serikali nzima. Wanafunzi wa siku hizi wanapewa swali halafu wanamfuata mwalimu ofisini kuuliza, hivi hili swlai lina maana gani? Hawa wanafunzi wanauliza hivi wakati vitabu vipo lakini wanaona tabu sana, unadhani kusahihisha upya matokeo kutashindwa kuwadekeza?, anasisitiza Zotto.
Anaongeza kuwa, “Iko wapi Lambart, ambacho ni mkate wa somo la Jiografia, Kozlov, Wadada na Budere, na Walter Rodney? Sisi tulisoma haya yote tukiwa kidato cha tano na sita na tulipoyaona Chuo hatukushangaa. Tuliweza kutoa mifano na kuthibitisha hoja mbalimbali, ndipo tukaanza kukariri kurasa hadi kurasa eti leo wanafundisha wanafunzi majibu na maswali, ndio vitabu vyao vya leo. Uwezo wa kufikiri kwa kupambanua (Analytical thinking) umepungua sana,”

Alipotakiwa kueleza ni kwanini anadhani kuna tatizo la kupungua kwa uwezo, akasema, “Nimesama hayo kwakuwa nimejiuliza kwanini miaka ya hivi karibuni watu wamemaliza shahada na wanarudi kuunganisha shahada ya pili. Wengne hata kazi hawataki, nikajiuliza, je, ni hamu ya kuongeza elimu tu? Kazi ni shida? Ushindani mkubwa au kupanda madaraja kirahisi? Nikagundua kuwa elimu yetu haijajitoleleza vizuri kutatua matatizo. Je, hizo shahada za pili zimesaidia kutatua kama haya ya matokeo ya wadogo na watoto wetu huko sekondari? Hapo jibu ni hapana,” anasema James Zotto.

“Tumepoteza, the purpose of education, ambayo Mwalimu Nyerere alituachia. Binafsi nilijiona nimekamilika baada ya kumaliza kidato cha sita kuliko hata nilipomaliza Chuo Kikuu, tuliandaliwa kujitegemea kujenga hoja na kufanya kazi, lakini sasa naona kabisa kuna ombwe kubwa,” anasema Zotto

Anaongeza kuwa, “Mwalimu Nyerere alitaka elimu yetu iwe imekamilika kila hatua na kila hatua imsaidie mhitimu atatue  matatizo yake na ya jamii. Je, darasa la Saba la leo, Kidato cha Nne, cha Sita, Cheti, Stashahada vinajitosheleza? Nafikiri tutasoma hata Uzamivu na itakuwa bado. Itabidi tutafute elimu kubwa zaidi ya Uzamivu huenda ikatosha. Tujikague.”

“Labda nikuulize swali la kizushi, ungesikia Dk Ndalichako katangaza daraja la kwanza wamepata wanafunzi asilimia 80 na sifuri hakuna, kisha wengine wamepata asilimia 20 wapo katika, je ungempongeza Dk Ndalichako? Lazima niwe mkweli katika hili la kufutwa mitihani kwa vile wanafunzi hawa wa siku hizi nawafahamu, pia nafahamu kuwa Dk. Ndalichako ni mtu kati ya wachache wanaoheshimu  taaluma zao, waliposema walikubaliana wapitishe matokeo na NECTA ikatoa sahabu zake, mbina hatuambiwi waliyokubaliana ni yepi? Je, ina maana kuna matokeo ya makubaliano na yaliyotolewa na NECTA? Ndugu yangu tuna matatizo kwenye familia na uendeshaji wa elimu, siasa imeingia na dini pia. Halafu wanafunzi wenyewe hawa wavivu na wazembe tutarajie nini kama kila siku wanamfuata Mwalimu ofisini kuuliza maana ya swali wakati vitabu vipo?” ansema Zotto.

2 comments:

  1. Mimi hapa najiuliza, kosa ni la nani, ni nani kasabaisha hadi ifikie hapo, `mwanafunzi kuwa mzembe'...tuliangalia hilo kwa undani zaidi, maana huyo mtoto amekuwa mikononi mwa walimu, miaka saba ya primary, na miine ya sekondari,....hatimaye kwenye mtihani huyo mtoto anafanya hayo yaliyofanyika.
    Tunahitajika kuangalia matokea haya, kwa mbali zaidi,....najiuliza, mzazi na mwalimu walikuwa wakishirikiana vipi hadi huyu mtoto akafikia hapo, kama mtoto anatoka nyumbani saa kumi alifajiri, anafika kwenye daladla, anafukuzwa, mpaka apate usafiri, ni saa tatu, anafika shuleni kachoka....haya hatuyaangalii.
    Haya anafika shuleni, mwalimu anapiga miayo ya njaa, hajui familia yake itakula nin, bado anatakiwa kuwasomesha hawa watoto, waelewe, na bado haruhusiwi hata kumchapa huyu mtoto mkorofi...
    Hakuna vitabu, ...makampuni mazuri yanajulikana dunia, yamefungiwa, mavitabu yanaharibia kwenye magodown, watu wanaangalia, maslahi yao tu....kweli mitihani ndiyo tunaitizama kama kigezo cha `uzembe ' wa huyu mwanafunzi?
    Mimi nahisi `uzembe' huu uwe ujumbe wa kuchimbua zaidi, tuangalia mizizi ya tatizo hili,....tusipozina ufa ....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu nimeandika ujumbe huu kwa haraka, naona makosa yapo mengi...si unajua tena kubana matumizi!

      Delete

Maoni yako