June 10, 2013

BINTOU YAWA SCHMILL; BONDIA WA KIKE MWAFRIKA NCHINI UJERUMANI


Unapozungumzia mchezo wa ngumi au ndondi nchini ujerumani Jina la Bondia wa kike mwafrika Bintou Yawa Schmill a.k.a "The Voice" ndiye anayemudu uringo "Boxing Ring" na kulipeperusha bara la Afrika ughaibuni.

Bondia  huyo kike  Bintou Yawa Schmill mwenye maskani kule Drackenburg nje kidogo ya mji wa Bremen,amekuwa kivutio kwa washabiki wa kimataifa na tishio kwa wapinzani wake anapokuwapo ulingoni.

Boxer Bintou Yawa Schmill mzaliwa wa Togo mwenye makao yake nchini ujerumani alianza kucheza ngumi akiwa na umri mdogo na kushinda mara 14 katika mashindan 24 na mara 4 K.O ,katoka draw mara 2 uzito wa Water weight 69 Kg, katika ngumi za ridhaa.

Kuanzia mwaka 2007 Boxer Bintou Yawa Schmill  a.k.a "The Voice" alihamua kucheza ngumi za kulipwa kwa uzito wa Water weight , amepigana na kushinda professional Record 4 na Ushindi wa K.O mara 3. Boxer Bintou Schmill kwa sasa kajiandaa kupambambana na bondia
yeyote yule wa kike na mahala popote  duniani


1 comment:

  1. HONGERA ZAKE, KWELI ANAONEKANA NI MOTO WA KUOTEA MBALI

    ReplyDelete

Maoni yako