June 06, 2013

SERIKALI KULETA MELI MPYA ZIWA NYASA

Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete imepanga kutumiza ahadi yake ya kuleta meli mpya katika ziwa Nyasa. Wakati akigombea urais, Jakaya Kikwete aliahidi kuleta meli mpya ambayo ingesaidia kufanya safari katika ziwa hilo na kurahisisha usafiri.

Kwa muda mrefu Ziwa Nyasa limekuwa likitegemea meli mbili, Mv Songea na Mv Iringa, lakini seikali imetangaza kuwa inatarajia kuleta meli kubwa mbili katika ziwa Nyasa.
Uamuzi huo una maana kuwa meli za Mv Iringa na Mv Songea hazitakuwa tegemeo tena. Meli hizo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa kutokana na ubovu unaojitokeza kila mara.
Hivyo wakazi wa Wilaya ya Nyasa wanatarajiwa kupokea meli ambayo inatawasaidia kusafiri badala ya kutegemea barabara ambayo bado ni mbovu huku magari yakishindwa kuwafikia wananchi wengi.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako