July 18, 2013

HII NDIO SIRI YA KUUAWA OSAMA



MASUALA mengi yanasemwa juu ya kifo cha Osama Bin Laden, lakini ni wachache wanajua hali halisi ya kitu kilichotokea.
Katika duru sasa siasa kumekuwa na sifa nyingi kwa kukamatwa hadi kuuawa, wapo watu wanashindwa kugundua kiini na sababu zote zinazoelezewa kwa kifo hicho.
Utawala wa Obama umefanya mambo makubwa sana katika siasa za Marekani huku akisifiwa kwa kutoogopa kuwatumia wataalamu wake kumkamata Osama.
Mimi naguswa na jambo ambalo linapotoshwa na wengi sana na watu wa Afrika Mashariki. Ninaandika nikiwa na sababu nyingi, sina haja ya kuona uongo ukisemwa wakati ukweli upo bayana. Kuna haja ya kuelezea hilo.
Wakati wa kutafutwa Osama Bin Laden kila kitu kipo wazi na hata baadhi ya filamu zimeruhusiwa na serikali ya nchi hiyo.
Kwa mfano, Ripoti ya mipango yote ya kumkamata iliwekwa wazi tangu alipouwawa baada ya kufanikiwa kutokana na kuikamata ‘network’ yake.
Taarifa za kuuawa Osama bin Laden zimetolewa mara nyingi mno na watuhumiwa watatu muhimu wa Al Queda waliwekwa kwenye gereza la Guantanamo, nchini Cuba.
Mtuhumiwa wa kwanza ni Khaleed Sheikh Mohamed (KSM), ambaye anatajwa kuwa ndiye alisuka mipango yote ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.
Baada ya kufichua siri za Osama, alisema kuwa mtu muhimu anayeunganisha mawasiliano yote ni Al Kuwait. Kuwait anatajwa alikuwa akibeba mipango yote ya maelekezo na mawasiliano kutoka kwa Osama na kupeleka kwa wanachama wengine wa Al Qaeda.
Mwingine ni Abu Zubeida ambaye kazi yake kubw ailikuwa ni kushirikiana na Ramzi Yousef ili mpango wa kulipua WTC kabla ya tukio la kuangusha minara miwili ya jengo hilo kwenye shambulizi kubwa zaidi la Septemba 11 mwaka 2001.
Gaidi Abu zubeida aliteswa sana shirika la kijasusi la Marekani (CIA) kwa kutumia EIT(Enhanced Interogation Techniques) kama kutumbukizwa kwenye maji.
Licha ya adhabu zote hizo awali alikataa kufichua siri za Osama, ndipo ukaandaliwa mpango kabambe ambapo CIA wakamtishia kumkabidhi kwa majasusi wa serikali ya Saudi Arabia.
Baada ya kuambiwa hayo, gaidi huyo hakuwahi kuogopa lolote na alikubali kupelekwa Saudi Arabia kutokana na sifa yao ya kutesa kupita kiasi.
Kwa ujanja wa hali ya juu CIA walifanikiwa kumhadaa gaidi huyo kwa kumpakiza kwenye ndege na kuzunguka naye muda mrefu angani wakijifanya wanampeleka Saudi Arabia, mwishowei walitua naye sehemu moja mafichoni huko Marekani ambapo maofisa wa CIA wa Kiarabu waliovalishwa mavazi ya Jeshi la Saudi Arabia wakumuuliza maswali hapo ndipo akamtaja Al Kuwait.
Baadaye aliwataja wafadhili wa Osama bin Laden akiwemo mmoja wa watoto wa mfalme wa Saudi Arabia, pamoja na Jenerali wa Jeshi la nchi hiyo na maofisa wengine wawili wa serikali.
Vilevile alitoa namba ya mtoto wa mfalme wampigie ili awaamrishe wamwachie. Watu wote waliotajwa na Abu Zubeida wakati akihojiwa CIA waliuawa kuanzia mtoto wa mfalme ambaye alikutwa amekufa akiwa kwenye mapumziko yake, huku yule Jeneral wa Jeshi alikutwa amekufa Jangwani kwa kiu na kukosa maji na wale maofisa wote.
Huo ndio ukawa mwanzo wa Osama kukosa msaada wa kifedha. CIA walianza kufuatilia nyendo za gaidi Al Kuwait nchini Pakistani, ambapo wakafanya mbinu za kumfuatilia kila alichokuwa akifanya ndipo wakagundua nyumba anaoyishi Osama huko Abbottabad, Pakistani.
Katika kipindi hicho Osama aliishiwa fedha na inaelezwa ilifika wakati hata wake zake walikuwa wakiuza mikufu na herein za dhahabu ili kupata fedha za matumizi.
Ofisa mmoja wa CIA ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye shirika la Save The Children lililokuwa lnafanya kampeni ya Kinga ya magonjwa ya watoto, alikodiwa nyumba iliyo karibu na nyumba ya Osama ili kukamilisha nyendo zake.
Hivyo basi siyo kwamba Marekani walikuwa wanachukua DNA za watoto na kulinganisha na za Osama. Bila shaka huo ni uongo kwa sababu kinga iliyokuwa inaratibiwa na Save the Children ilikuwa ni ya matone, kwahiyo kuwapa watoto matone huwezi kupata vipimo vya DNA.
Mpaka sasa CIA wanamtafuta kamanda wa pili wa Al Qaeda, ambaye pia ni daktari wa Misri, Ayman Al Zawahiri. Huyu Zawahiri  naye inaaminika amejificha kwenye mpaka wa Afghanistan na  Pakistan.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako