July 06, 2013

FILAMU ZETU NA UTATA WA MAJINA-1


Tasnia ya filamu hapa nchini imewezesha upatikanaji wa ajira, hii ina maana kuwa tasnia hii imesaidia kuibua vipaji na kusaidia kupunguza tatizo hilo. Pamoja na hali hiyo bado kuna mambo muhimu yanatakiwa kurekebishwa.
Hebu tujadili jambo dogo, aghalabu limekuwa likizua utata katika majina ya filamu na dhima hali ya filamu husika.
Kuna suala la uteuzi wa majina ya filamu, ili kuwakilisha ndoa ya fani na maudhui. Nitatoa mifano michache; filamu moja inaitwa ‘

The Beginning of All”. Kwa tafsiri ya watunzi na waigizaji wake kwa lugha Kiswahili “Mwanzo wa yote”. Kwa vyovyote vile huo ni utata. Swali la kwanza; “mwanzo wa yote” ni kitu gani?
Nini lengo la mtayarishaji na mwandishi wa muongozo wa filamu husika? Katika sarufi maana (semantic meaning), hilo linaweza kuwa suala la kawaida au linaloeleweka. Lakini katika sarufi miundo ni vigumu kuisema “The beginning of All” ndio utungaji wa sentesi ama neno sahihi.
Hakuna kitu kama “mwanzo wa yote” bali ilipaswa kusemwa “mwanzo/chanzo”, sababu huo ni mwanzo wa jambo, kitu, suala ama vyovyote vile. Kwahiyo sio kweli kusema  “The Beginning of all”.

Filamu nyingine inaitwa “End of the day”. Wapo wengine wanaweza na kuanza na “at” yaani “At end of the day”. Neno “at” ni miongoni mwa “preposition”. Lakini sijawahi kuona neno hilo linaweza kuwakilisha ama kusimama kama neno sahihi la mwanzo wa sentesi, bali hutumika kama sehemu ya sentesi kuelezea somo pengine, ‘compliment of subject’.

Sasa hii ‘End of the day” inatafsiriwa kuwa “Mwisho wa siku”. Sio kweli katika tafsiri hiyo, hakuna neno katika Kiswahili linalosema “Mwisho wa siku” bali ilipaswa kuwa ‘Mwishowe’ ‘Hatimaye’, au ‘Tamati’.

Hata kama kutakuwa na utetezi wa majina ya yenye mvuto, lakini lazima kanuni za lugha ziwekwe mbele zaidi ili kuendana na matumizi yake. Filamu nyingine inaitwa ‘Zawadi ya birthday”. Hapa tunakuta mgogoro wa jina, ni lugha gani ilipaswa kutumika.

Je, haikufaa kutumia neno “Zawadi” ama tafsiri rahisi yenye lugha moja? Ukiangalia jina la filamu hiyo ina maana tunakutana na mgogoro wa matumizi ya lugha, maana inakuwa mchanganyiko wa lugha yaani ‘code mixing’.

Kwanini tunafika hatua hii ya kutoheshimu lugha? Ndio maana nasema ni utata huo na inaleta shida kwa wapenzi wa lugha moja kuwaelewa wasanii wetu. Pengine utakuwepo utetezi kuwa wanalenga soko la kimataifa, ni kweli lakini lugha yako ndio msingi wa kukufikisha kimataifa.

Kwa mfano filamu inaitwa “Hidden Truth” kwa lugha rahisi yaani wanaotafsiri kwa njia mbaya utasikia “ukweli uliyofichwa”.

Usahihi wake ni  “ukweli. Ni siri tu kama ipo au imejulikana haiwezi kusemwa siri iliyofichwa, bali imeshajulikana hivyo inabaki kuwa na haiondoi mantiki ya “ukweli’. Zipo filamu zingine zinakuwa na majina ya ajabu.

Pengine watunzi wanapotunga wanakusudia au wanakuwa na wazo la ujumbe tu, hawazingatii maneno wanayotumia kufikisha ujumbe kwamba yanaleta mkanganyiko. Kwa mfano “Night Blindness”, je nini dhumuni la jina kama hilo. Nafikiri tunaweza kusaidiwa kupata mwafaka wake.

Kuna suala la kunakili majina na kuleta utata kwa wapenzi wa filamu, kwa mfano filamu za ‘Deception’, imechezwa na marehemu Steven Kanumba na Rose Ndauka, lakini jina la filamu kama hiyo lilishawahi kutolewa na waigizaji Michelle Williams, Hugh Jackman, na Owen Macgregory.

Nyingine ni hii ‘Wicked Love’ iliyochezwa na Vincet Kigosi akiwa na Aunt Ezekiel, pia filamu yenye jina hilo hilo iliwahi kutolewa na waigizaji Vinci Colosimo na Rebecca. Vipi kuhusu filamu za ‘The Bestman’? Pia This is it’ ambapo Michael Jackson alitoa mkusanyiko wa matamasha yake na kuweka kwenye ‘video’.
Tukumbuke nimetumia hoja mbili; kwanza tafsiri potofu katika maneno yanayobeba majina ya filamu na filamu zenye utata kwa kufanana majina.
Inaendelea hapo chini ………………

No comments:

Post a Comment

Maoni yako