August 24, 2013

MABADILIKO RASMI YA BARABARA KUU KUTOKA MBINGA HADI LIULI, KWA MAENEO YA WILAYA YA NYASA


Na Vitus Matembo, Mbamba Bay

Kama inavyofahamika kuwa Wilaya ya Nyasa ipo kwenye mchakato mrefu wa mabadiliko ya maendeleo ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kutokana na vitutio vilivyoko kwenye wilaya hii. 

Harakati za kiserikalina watu mbalimbali katika wilaya Nyasa zimeshika kasi huku wananchi wakichangamka zaidi. Lakini baada ya bomoa bomoa iliyotokea miezi kadhaa iliyopita, kwa sasa kuna jambo jingine kuhusu Barabara ya kutoka wilaya Mbinga hadi wilayani hapa, Nyasa.

Barabara Kuu unapotokea Mbinga itachepukia Nangombo, Ndesule, Chipilimba na kuingia Ndengele. Agosti 23 kulifanyika malipo ya fidia kwa wakazi wa maeneo hayo. Hata hivyo kuna jambo moja linalochanganya hadi sasa kwani Hoteli mbili za vigogo wa wilaya hii hazijabomolewa kadiri ya ramani inavyotaka kwani ziko barabarani.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako